Na Haji Nassor, Pemba
WATU sita wanaodhaniwa kuwa ni wavuvi
raia wa Comoro, ambao wameondoka kwao tokea Mei 11 mwaka huu na kukaa baharini
wakiwa na chombo chao siku 45, wameokotwa jana katika bahari ya Matumbulini
wilaya ya Mkoani Pemba.
Watu hao waliokotwa na wavuvi wa shehia ya
Mwambe wilayani humo, wakati walipokuwa kwenye kazi zao za uvuvi, ndipo
waliopoona ishara ya nguo zikipeperuka baina ya majira ya saa 4:00 na saa 5:00
usiku na walipowafika walikuta watu hao kutoka Comoro.
Taarifa
zinaeleza kuwa baada ya kuokotwa wakiwa wana elea elea na chombo chao aina ya
‘Fiber’ walifikishwa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani majira ya saa 6:00 usiku
na kuanza kutiwa majia na kisha kufanyiwa uchunguuzi wa afya zao.
Akizungumza
na waandishi wa habari hizi hospitali hapo, Muuguzi wa afya ya akili wa
hospitali hiyo, Dk. Said Ali Said alikiri kuwapokea watu hao, ambapo alisema
baada ya uchunguuzi wamegundua kuwa watu hao walikuwa wamekosa nguvu baada ya kukosa
chakula kwa muda mrefu.
“Unajua
tumegundua kuwa, wamekosa nguvu mwilini, maana wamekaa na njaa kwa muda mrefu,
ingawa samaki wa kukausha kwa jua waliokuwa wanakula, kidogo wamewasaidia kwa
hivyo hakuna alieathirika’’,alifafanua.
Alifafanua
kuwa mara baada ya kuwatia maji, waliwapatia uji, chai na mikate, ambapo afya zao
zilianza kujirudia kama kawaida na kwa sasa wanaendelea vyema.
Aliwataja
watu hao waliojiita wavuvi kuwa ni, nahoza Alloui Huomad Mromaji (40), msaidizi
nahoza Yunus Maishe Mussa (45), Deiyan Ahamad Wali (25), Hassan Mmadi Abdul
(59), Ibrahim Mzee Said (45) na Abdalla Abdurr-ahaman Abass (35) wote wakaazi
wa visiwa vya Comoro.
Akizungumza
na waandishi wa habari msaidizi nohoza wa wavuvi hao ambae anazungumza lugha ya
kiswali kidogo, Yunus Maishe Mussa, alisema hawakuwa katika mavuvi siku hiyo,
bali walikumbwa na mkasa huo walipokuwa wakirudi kununu chakula.
“Hii
ni boti yetu ya uvuvi, lakini hiyo tarehe hiyo 11 ,wezi Mei, tulikuwa tunatoka
kisiwa kimoja kwenda chengine, ndipo tulipoishiwa na mafuta na kubururwa na
maji hadi Pemba’’,alifafanua.
Alieleza
kuwa hawakuja kisiwani Pemba kwa nia mbaya, bali ni kutokana na upepeo unavyo
vuma, ndio maana wamejikuta kisiwani humo jana, baada ya kukaa baharini siku 45
na kuokotwa na wavuvi wenzao.
“Kipindi
chote hicho tulikuwa tunakausha samaki kwa jua, na kisha tunakula, ndio chakula
chetu hatuna chengine, hadi tullipoletwa juu bandari ya Mkoani’’,alifafanua.
Afisa
Uhamiaji wilaya ya Mkoani Pemba Abdalla Shehe alisema, wanaendelea kufuatilia
taarifa za watu hao, kwanza kujua iwapo ni wavuvi na baada ya kujiridhisha
watawakabidhi kwa ubalozi mdogo wa Comoro uliopo Zanzibar kwa kuwarejesha kwao.
Hata
hivyo alisema wanamashaka kidogo kwa vile kama ni wavuvi walipaswa waone sehemu
maalumu ya kuhifadhia samaki, na kukosekana ndani ya chombo hicho, ndio maana
hawajaridhishwa na kauli zao.
“Tunafanya
mawasiliano ya kimataifa, kujua kwamba kwenye nchi yao kuna taarifa za kupotea
wao, na kisha na sisi baada ya uchunguzi wetu kukamilika na kujiridhisha tutawasiliana
na ubolozi kwa hatua’’,alifafanua.
0 comments :
Post a Comment