JANUARY MAKAMBA: NANI NI NANI URAIS CCM?
HISTORIA YAKE
January Makamba ni mmoja kati ya vijana machachari katika siasa za Tanzania akiwa na sifa kubwa ya kuendesha siasa za kisasa na zinazowavutia vijana wengi. Makamba alizaliwa Januari 28, 1974 mkoani Singida (ana miaka 41 sasa) na ni mtoto mkubwa kati ya watoto wanne wa Mzee Yusuph Makamba. Kwa sasa January ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Yusuph Makamba (baba) ni mwanasiasa nguli na mwenye jina kubwa hapa Tanzania akishikilia nyadhifa nyingi ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Makamba amestaafu siasa akiwa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM. Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na ukuu wa mikoa kadhaa kwa nyakati tofauti. Mama mzazi wa January anatokea Mkoa wa Kagera na baba yake anatokea Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
January alisoma katika Shule za Sekondari Handeni na Galanos mkoani Tanga na kisha akaendelea na kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Forest Hill. Alijiunga na Chuo cha Quincy huko Massachusetts, Marekani kisha akajiunga Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana kilichoko Minnesota - Marekani na kusomea masomo ya amani (peace studies).
Baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza aliendelea na shahada ya pili (uzamili) ya sayansi akibobea katika Uchambuzi na Usuluhishi wa Migogoro kwenye Chuo Kikuu cha George Mason – Marekani, mwaka 2004.
Aliporejea nchini, January alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa Ofisa wa Daraja la Pili. Nyota yake ilianza kung’ara kisiasa pale aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Jakaya Kikwete alipoteuliwa na CCM kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. January alijiunga na timu ya kampeni ya Kikwete na kusafiri na “rais mtarajiwa” nchi nzima.
Baada ya Kikwete kuingia Ikulu, alimteua January kuwa msaidizi wake katika nafasi ya “Msaidizi Binafsi wa Rais Katika Mambo Maalumu”. Alitumikia wadhifa huo kuanzia mwaka 2005 – 2010.
MBIO ZA UBUNGE
Aliingia rasmi kwenye siasa mwaka 2010 kwa kuomba ridhaa ya CCM kuwa mbunge wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto.
Kwenye kura za maoni za chama hicho, alimshinda mbunge mzoefu, William Shelukindo kwa kupata kura 14,612 dhidi ya 1,700 za Shelukindo. Baada ya kushinda ndani ya chama chake, January hakukutana na mpinzani yeyote kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na hivyo akaingia kwenye rekodi ya wabunge waliopita bila kupingwa.
Katika Bunge la 10 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na mwaka 2011 chama chake, CCM, kilimteua kuwa katibu wa siasa na uhusiano wa kimataifa akichukua nafasi ya Benard Membe. Alitumikia wadhifa huo ndani ya chama chake hadi mwaka 2012 alipomuachia Dk Asha-Rose Migiro.
Katika Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, January alichaguliwa kuwa kati ya wajumbe 10 wa kamati kuu ya chama hicho kikongwe kutokea upande wa Tanzania Bara akipata kura 2,093.
Mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. January ni kati ya wabunge walioanzisha mifuko maalumu kwa ajili ya majimbo yao, mfuko wake unaitwa “Mfuko wa Maendeleo wa Bumbuli” ulioanzishwa Julai 2012 ukiwa na jukumu la kutafuta nyenzo na mapato ya ziada ya kusaidia miradi mbalimbali kwenye jimbo hilo.
MBIO ZA URAIS
Hadi mwaka 2012, January hakuwa na mipango ya kugombea urais, aliwahi kuhojiwa katika kipindi cha mikasi cha televisheni ya EATV, Machi 2012 na kusisitiza kuwa hana mpango na urais lakini Februari, 2014 watu wengi walishtushwa na “onyo” lililotolewa na vikao vya chama chake dhidi yake na wanachama wengine watano kuwataka wasiendelee na “mchezo” wa kampeni za urais kabla chama hicho hakijaanzisha mchakato huo rasmi, ndipo wengi wakaanza kuhisi kuwa naye anausaka urais.
Julai 2, 2012, January aliweka bayana nia yake wakati anahojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, akisisitiza kuwa ni lazima agombee urais kwa sababu Tanzania inamhitaji mtu mwenye sifa kama zake na mtu wa kizazi cha sasa.
Tangu wakati huo, January amefanya mambo mengi ya kuelekea kwenye nia yake hiyo ikiwamo kutoa kitabu maalumu cha maswali 40, kilichoandikwa na mwandishi Privatus Karugendo kikionyesha maswali na majibu ya namna kijana huyu wa kisasa atakavyoweza kupambana na changamoto za urais iwapo chama chake kitampa ridhaa na Watanzania wakamchagua.
NGUVU YAKE
January ni kijana kwa umri na kwa yale ayasemayo. Pia, ikumbukwe kuwa mwaka huu kuna vijana lukuki ambao watapiga kura kuliko wakati mwingine wowote, kwa hiyo chama ambacho kitampitisha rais kijana kwa umri, mwonekano na hata mipango, kina nafasi kubwa ya kuchukua kura nyingi za vijana.
Elimu yake na uzoefu wa kufanya kazi serikalini na Ikulu ikiwa ni pamoja na kuzunguka nchi akijifunza matatizo ya Watanzania ni kati ya mambo muhimu yanayojenga nguvu za January, lakini yote haya hayawezi kuchukuliwa kama uzoefu mkubwa zaidi kumsaidia katika nyanja za uimara wa kiongozi mtarajiwa wa nchi.
Lakini pia nguvu ya baba yake ambaye ameshatangaza wazi kumuunga mkono mwanaye, nayo ni turufu nyingine. Wale waliokuwa wanazikubali siasa za Mzee Makamba watakuwa nyuma yake.
Ni wazi kuwa Mzee Makamba ana mtandao mkubwa na anaweza kutumia mtandao huo kumsaidia mwanaye, January.
UDHAIFU WAKE
January ni kiongozi mwenye mitizamo “tata”. Kuna wakati amewahi kusikika akitamka kuwa “…..Moja ya vitu vitakavyozuia rushwa ni adhabu kali ambayo itaonekana. Kwa nini madikteta wanawaua watu hadharani? Wanachojaribu kukionyesha ni kwamba kama siku moja mtu akijaribu kuwapindua atapelekwa uwanjani na kupigwa risasi hadharani. Lengo ni kuwatia watu hofu.”
Kauli ya namna hii ni hatari kwa kiongozi ambaye anahitaji kuongoza nchi inayoendeshwa kiimla katika baadhi ya masuala na inayopigana kurekebisha nguvu ya demokrasia yake na kuondoa dhana za u - imla.
Mataifa ya sasa yanapigana kusaka haki na kuona haki inatendekea, hayafurahii watu kuuawa na kutawaliwa na madikteta, kauli hii imewahi kujadiliwa na kukosolewa na wachambuzi wengi na January mwenyewe hakuwahi kuirekebisha. Kwa hiyo kwa upande mmoja, anaamini katika demokrasia lakini kwa upande mwingine, anaamini ‘udikteta’. Kwa bahati mbaya, Tanzania haihitaji rais ‘dikteta’ na kufikiri namna hiyo ni udhaifu mkubwa.
Katika Bunge Maalumu la Katiba (BMK), January aliwachukiza vijana wengi wanaomuunga mkono baada ya kuonekana akitetea hoja za Serikali yake hata kama hazikuwa na mashiko.
Jambo hili lilitarajiwa kufanywa na watu wenye umri mkubwa na wanaotetea mfumo uliopo “status quo”. Vijana wenzake kama Ridhiwani Kikwete na Mwigulu Nchemba waliweka misimamo yao katika baadhi ya masuala ya msingi, kwa mfano, Ridhiwani alisisitiza kuwa mchakato ukiendelea bila maridhiano unakuwa haramu.
Hata bunge liliporejea kumalizia kazi, Nchemba alihoji kwa nini fedha za umma ziendelee kutumika kupitisha katiba ambayo haina maridhiano?
Vijana kama January walipaswa kusimamia jambo hili ili jamii ione kuwa wanaweza kuwa viongozi wajao na wasiofuata mkumbo na matakwa ya vyama vyao. Kwa hivyo, January ana taswira ya “ki - chama” kuliko “ujana” na anaweza kuwa rais atakayetetea chama chake zaidi kuliko matakwa ya wananchi kama alivyofanya kwenye BMK.
NINI KINAWEZA KUMFANYA APITISHWE
Ukaribu wa January na Rais Kikwete unatajwa kuwa faida inayomfanya ajione ana nafasi ya kuvuka baadhi ya vizingiti. Watu hawa walifanya kazi pamoja Wizara ya Mambo ya Nje, wakafanya kazi pamoja Ikulu na baadaye wameendelea kufanya kazi pamoja serikalini na ndani ya CCM wakionekana kuwa watu walioshibana. Ukiwa unataka kuongoza nchi na kisha una ukaribu na maelewano na rais aliyepo madarakani hilo ni jambo muhimu sana kwako.
January anajionyesha kama kiongozi wa kisasa, anazungumzia hoja za usasa zaidi kuliko ukale na anasimamia masuala kadhaa vizuri pale anapopewa nafasi. Wakati anaongoza Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini alikabiliana na wizara hiyo vilivyo katika tatizo la mgawo mkali wa umeme. Msimamo wake ulikuwa ni kutafuta suluhu ya tatizo hata ikiwezekana baadhi ya masilahi ya wafanyabiashara na viongozi wa Serikali kuguswa. Msimamo wa wakati huo ulimuweka shakani kiuhusiano na vigogo wengi wa sekta hiyo lakini hakujali.
Nilisahau kusema kuwa January ni kijana anayevutia “handsome”. Wanasiasa wa namna hii huuzika kirahisi majukwaani na huwapumbaza wapigakura walio wengi. Uzuri wa mtu, tabasamu lake, ucheshi wake na mvuto wake wa nje hutafsiriwa kama kioo cha usafi wa roho na uadilifu, hata kama vivutio hivyo haviakisi hali halisi ya ndani.
Umakini na uadilifu ni masuala mengine ya msingi aliyonayo na hata Rais Ali HassanMwinyi kwenye dibaji ya Kitabu cha Karugendo cha Maswali 40 juu ya January Makamba, amemuelezea mwanasiasa huyu kama “kijana makini”.
NINI KINAWEZA KUMWANGUSHA?
Kati ya mambo yanayoweza kumwangusha January katika mbio zake za kusaka urais ni suala la Kuhukumiwa kwa umri (ujana). Ujana una changamoto zake katika siasa za Afrika, bara ambalo baada tu ya uhuru, lilisahau harakati za vijana wengi waliolikomboa na kuanza kukasimu madaraka kwa wazee wenye umri mkubwa kwa kisingizio cha “busara za wazee”. Ikiwa CCM itampima kwa kigezo cha umuhimu wa wazee au vijana kwenye kuongoza Ikulu ya nchi, hukumu hiyo inaweza kumuweka nje ya ulingo.
Udhaifu mwingine ni mtandao duni. January hana mtandao wa maana ndani ya CCM na hata nje ya chama chake si mtu wa kujadiliwa katika nafasi hii muhimu. Ili uwe kiongozi wa kisiasa, unahitaji kuwa na mtaji na nguvu ya watu, jambo hili amelikosa na kwa hiyo matarajio yake ya kupitishwa na chama chake ni madogo pia.
Jambo la tatu litakalomuangusha ni kukosa fedha za kutosha. Kwa umri wake, huwezi kusema ana “mapesa ya kutosha”. Hana fedha za kutisha kusaka ridhaa ndani ya CCM. Ukweli halisi ni kuwa, mtu asiye na fedha za kutosha au mitandao ya matajiri wenye fedha za kutosha anakuwa na nafasi ndogo ya kupenya tundu la mchujo wa CCM ili hatimaye agombee urais kupitia chama hicho.
Kwa bahati nzuri, January alishiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumsaidia Kikwete kupenya ndani ya chama chake mwaka 2005. Anajua namna Kikwete alivyokuwa amezungukwa na “mtandao mzito” wa watu wenye fedha zao wakati anasaka nafasi hiyo. Anajua nguvu ya fedha ndani ya chama chake kama turufu ya kumuongezea nguvu mgombea, kukosa fedha kunampunguzia nafasi ya kuwashinda wagombea wengine waliojipanga vizuri kwenye eneo hilo.
Jambo la nne linaloweza kumkwamisha January Makamba ni taswira ya baba yake mzazi. Mzee Makamba anaweza kuwa na mtandao mkubwa, lakini katika mtandao huo kuna watu wanaomkubali na wanaomchukia kwa sababu mbalimbali. Hivyo, kama ilivyo kwa wanaoweza kumuunga mkono kutokana na ushawishi wa baba yake, pia wapo watakaompinga kutokana na mzazi wake huyo hivyo, inawezekana “akatwishwa mzigo mzito” ambao haukumstahili, lakini hiyo ndiyo hali halisi.
Lakini pia ripoti ya uchunguzi wa kusuasua kwa CCM iliyoratibiwa na kuwasilishwa na mwana CCM aliyepewa jukumu hilo mwaka 2011, Wilson Mukama, iliweka bayana kwamba Yusuph Makamba (wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa CCM) ni mmoja wa watu waliosababisha mkwamo wa CCM na kwamba alikuwa katibu mkuu asiyewajibika, aliyependa makundi na misuguano na viongozi wenzake bila sababu.
Taswira ya Mzee Makamba inaweza kumhukumu kijana wake katika siasa za Afrika ambako huwa inaaminika kuwa ‘mtoto ni zao la baba yake’. Pamoja na Makamba Jr kujitenga na siasa na ukale za baba yake na hata baba yake kuonyesha kuwa anajiweka mbali na mwanaye, wachambuzi wa mambo wanaiona hiyo kama janja tu na kwamba huenda baba na mwana wana mipango ya pamoja ambayo baadaye inaweza kumfanya mwana naye awe na mitizamo ya baba yake enzi za uongozi wake, ukizingatia kuwa aliyemsimamia January katika safari yake yote na kumpigia “chapuo” huku na kule ni baba yake. Tayari Mzee Makamba ametangaza kumuunga mkono January katika safari yake ya kuwania urais.
Kuhusishwa huku kwa January kwenye taswira ya baba yake ni jambo hatari kwake lakini linaloepukika ikiwa litafanyiwa kazi na kuwafanya watu watambue kuwa makosa ya baba si ya mwana, akishindwa kwenye kuwashawishi wana CCM kwenye eneo hili ina maana maadui wa baba yake kisiasa watakuwa pia maadui wa January katika safari yake.
ASIPOPITISHWA (MPANGO B)
Namuona January kama kijana mwenye mipango ya muda mrefu na kwamba iwapo hatapitishwa na chama chake, atagombea ubunge katika Jimbo la Bumbuli na kutegemea nafasi za Baraza la Mawaziri katika Serikali ijayo (iwapo itaundwa na CCM) na kisha namuona kama mwanasiasa mwenye nguvu kubwa na labda mmoja wa wasaka “uteule” wa kugombea urais ndani ya CCM mwaka 2025.
HITIMISHO
Makamba ni kijana wa kupigiwa mfano katika baadhi ya masuala muhimu ambayo amewahi kuyasimamia na yaliyoko kwenye historia yake, ni hazina ndani ya CCM. Namuona mwanasiasa huyu kama “mmoja wa watu muhimu wa kutegemewa” ndani ya CCM kwa miaka inayokuja.
Lakini kwa hali ya kisiasa na ya changamoto zinazoikabili nchi kwa sasa na kwa namna CCM ilivyozidiwa na changamoto ya Ukawa, nadhani inaweza kumkimbia na kutafuta mtu mwingine aliyejijenga zaidi.
Pamoja na kwamba nampa nafasi ndogo ya kupenya katika tundu la sindano, namtakia kila la heri katika kutimiza ndoto na azma yake ambayo ameipanga na kuipigania kwa muda mrefu sasa.
KUHUSU MCHAMBUZI:
Julius Mtatiro ni Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii, ana uzoefu mkubwa wa uongozi wa kisiasa hapa Tanzania. Ana Cheti cha Juu cha Sarufi na Lugha, Shahada ya Sanaa “B.A” katika Elimu (Lugha, Siasa na Utawala), Shahada ya Uzamili ya Utawala na Uongozi (M.A) na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (L LB) – Anapatikana kupitia +255787536759,(juliusmtatiro@yahoo.com) Uchambuzi na huu unatokana na utafiti na maoni binafsi ya mwandishi). (Uchambuzi huu umechapishwa na Gazeti la Mwananchi la Jumatano, 29 Aprili 2015).
KWA MAHITAJI YA BLOG PIGA 0714557223 SASA HIVI ILI UJIPATIE BLOG YAKO KALI NA YENYE MVUTO

0 comments :
Post a Comment