Muft Zubair Kayongo alikuja nchini Tanzania kwa matembezi ya kiofisi,lakini wakati alipokuwa nchini aliumwa na kuzidiwa ghafla hivyo akawaishwa hospitali ya Agha khan ambako alikuwa kipatiwa mpaka hapo leo alipofikwa na umauti.
Muft Zubair Kayongo alikuwa anasumbuliwa na kisukari pamoja na pressure ya kupanda .
Kwa mujibu wa shekh Kirya mwili wa marehemu utapelkwa katika msikitini huko Dar es salaam kwa ajili ya kuswaliwa kisha utapelkwa Uganda kwa ajili ya Mazishi.
Muft Zubair Kayongo aliingia madarakani baada ya muft aliyekuwepo shekh Shabani Ramdhani Mubajje kuonekana kuwa mbadhilifu kwani inasemekana alikuwa akiuza mali za waislam.
Hata hivyo Mubajje aligoma kuachia madaraka baada ya mashtaka hayo ya yeye kutokuwa muadilifu,na ndipo mwaka 2009 Shekh Zubair Kayongo alipotangazwa kuwa muft katika msikiti wa Kibuli na waislam ambao waliokuwa kinyume na Muft wa Uganda Shabani Ramadhani Mubajje
SOURCE:NEWSVISION
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment