Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut-Tahrir
Afrika Mashariki imeshutushwa na mauaji ya wanafunzi 147 huko Garissa,
Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Shambulizi hili limehuzunisha wengi
nchini Kenya hasa iki-zingatiwa limekuwa la kutisha zaidi hata kuliko
yote yaliyofanywa miaka ya hivi karibuni yakiwemo ya Westgate na
Mpeketoni. Huku tukishuhudia umwagikaji huu wa damu za watu wasokuwa na
hatia tungependa kutaja yafuatayo:-
1-Lawama lazima kwanza itupiwe vyombo
vya usalama ambavyo licha ya kudaiwa kufanywa mabadiliko ikiwemo hata
kubadilishwa kwa vinara wake bado mauaji kama haya yanaendelea. Twasema
ni jukumu la kiserikali kuhakikishia usalama wa raia wake wakiwa
madukani, mashuleni na barabarani. Hata hivyo twaonya kuwa tukio
lisichukuliwe kama njia ya kueneza chuki baina ya Waislamu dhidi ya
wasokuwa Waislamu au baina ya kabila moja dhidi ya kabila jengine.
2- Ama kukiri kwa Al-Shababu kuhusika na
shambulizi hilo sio muhimu bali la muhimu zaidi ni kuangalia na-tija
itakayotokamana na shambulizi hilo. Tumeona baada ya mashambulizi kama
haya jinsi gani vyombo vya usalama vya serikali vinavyotia Waislamu
kwenye misuko misuko zaidi kwa kile kiitwacho vita dhidi ya misimamo
mikali na ugaidi kwa ujumla. Pamoja na hayo, Mataifa ya kimagharibi
hufanya mashambulizi kusudi ili kusukuma ajenda zao za kikoloni katika
mataifa mbali mbali. Na kwa sasa twaona mataifa haya yanapatiliza
mashambulizi haya kama njia ya kufanikisha ajenda hizo zao za kikoloni
hasa ikizingatiwa kuwa kumegunduliwa katika kanda ya Afrika Mashariki
maadini mengi ikiwemo mafuta. Na hii ndio maana Uinge-reza ilitabiri
uwezekano wa kutokea kwake huku Marekani ikatahadharisha Uganda juu ya
uwezekano wa shambulizi la ugaidi. Kwa kifupi ni kuwa Mataifa ya
kimagharibi yana piga vita Uislamu kote dunia na hutafu-ta visingizio
vingi katika kampeni yake hii.
3-Tunaamini kuwa Kenya ingekuwa na sera
nzuri ya kigeni na ya kindani basi labda tusingeshuhudia mauaji haya.
Serikali yoyote ile inayolenga kudumisha amani kwa raia wake lazima
ihakikisha kuwa sera zote ni nzuri. Kwa bahati mbaya leo, sera za
mataifa mengi leo barani Afrika ikiwemo Kenya ni mbovu na huathiriwa na
mataifa ya Kikoloni ya Kimagharibi zilizo na sera mbovu zaidi za
kukoloni mataifa mengine. Ni kupitia sera hizi mbovu Marekani na
Uingereza hung’ang’nia rasilimali za Somalia huku mataifa hayo yakidai
yanapambana na ugaidi! Isitoshe mataifa haya hushawishi nchi nyingi ati
kusaidia vita dhidi ya ugaidi ambavyo mara nyingi husababishia hasara
kubwa kama hii tunayoshuhudia kwa sasa. Na hili liko wazi kwani wakenya
wengi kwa sasa hawana imani na oparesheni ya kijeshi ya Kenya huko
Somalia.
4-Tunamaliza tukisema kuwa Uislamu
unataka damu, mali na cheo kuheshimiwa. Hii ndio maana uka-haramisha
umwagikaji wa damu wa watu wasokuwa na hatia na ukaitaka serikali yake
(Khilafah) kulinda usalama wa raia wake wote pasina na kuangalia dini,
rangi au jinsia. Nasi Hizb ut-Tahrir tunalingania Uislamu kama mfumo
kamili wa kimaisha kwa lengo kuregesha maisha mazuri ya Kiislamu chini
ya Serikali ya Khilafah itakayohifadhi damu, mali na cheo kwa kila raia
wake sawa wawe ni Waislamu au wasokuwa Waislamu.
Kumb: 11/1436 16 Jumada Thaaniya 1436 Hijri 03 -4-2015
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki
Simu: +254 720597841 / +254 789 754 608Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki
Pepe: media@hizb-eastafrica.com
Tovuti rasmi ya Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.info
0 comments :
Post a Comment