Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
‘TP Mazembe FC ililala 1-0 ugenini dhidi ya Mamelodi Sandowns nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.’
Mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta amethibitisha kuwa ni
mkali baada ya kutupia na kuivusha TP Mazembe katika hatua ya 32 Bora ya
michuano ya Klabu Bingwa Afrika katika mechi yao ya leo waliyoshinda
3-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Uwanja wa Stade du TP
Mazembe nchini DR Congo.‘TP Mazembe FC ililala 1-0 ugenini dhidi ya Mamelodi Sandowns nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.’
Kwa matokeo hayo, Mamelodi Sundowns wametupwa nje ya michuano hiyo ya CAF kwa kipigo cha jumla cha mabao 3-2.
Ramahlwe Mphahlele alipata nafasi ya kuonesha mwanzo mzuri wa mechi, lakini akapiga pembeni kidogo mwa lango na kunyima Mazembe uongozi wa mechi.
Nafasi nzuri ya Sundowns kupata bao ilikuwa dakika ya 20 Teko Modise shuti la mbali la Robert Kidiaba lilipopaa katikati ya lango la Mazembe.
Wenyeji walipata bao dakika ya 28, lakini refa msaidizi alinyosha kibendera ya kuotea.
Mazembe walianza kufanya kweli dakika ya 36 kupitia kwa mkali wa mabao Rainford Kalaba, na kuzifanya timu hizo ziwe sare ya 1-1 katika mechi zote mbili (on aggregate).
Samattta alipeleka habari mbaya kwa kikosi cha Pitso Mosimane baada ya kuwafungia wenyeji bao la pili muda mfupi kabla ya mapumziko.
Hata hivyo, wenyeji walionekana kutoridhika na bao hilo Roger Assale alipowafungia la tatu dakika tatu kabla ya saa ya mchezo (dakika ya 57)
Sundowns walifanikiwa kupunguza bao moja dakika ya 84 kupitia kwa Percy Tau, aliyemalizia kazi nzuri ya Niang.
Hata hivyo, mabingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) hawakufanikiwa kupata bao la pili muhimu ambalo lingewavusha katika dakika zote zilizokuwa zimesalia baada ya kjuwa wamepata bao lao pekee la leo.
Vikosi kwa mujibu wa mtandao wa Soccer Laduuuma, vilikuwa:
TP Mazembe: Kidiaba, Frimpong, Kimwaki, Coulibaly, Kasusula, Diarra, Adjei, Asante, Assale, Samatta, Kalaba
Mamelodi Sundowns: Onyango, Schut, S. Zwane, Mphahlele, Mashaba, Kekana, Zungu, T. Zwane, Modise, Malajila, Billiat
0 comments :
Post a Comment