-->

SERIKALI YAOMBA RADHI KUSITISHA KWA MUDA TANGAZO LA AJIRA ZA WALIMU WALILOTOA JANA TAREHE 27/4/2015


OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM -TAMISEMI)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOLEWA KWA MUDA KATIKA TOVUTI ORODHA YA WALIMU WA MASOMO YA SANAA NA BIASHARA WA SHULE SEKONDARI-
AJIRA MPYA MWAKA 2014/15
Orodha ya wahitimu wa shahada na stashahada waliopangiwa katika
halmashauri mbalimbali inafanyiwa marekebisho baada ya kubainika
kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (Sebastian Kolowa University College-SEKUCO) cha Lushoto uliwasilisha orodha ya wahitimuwapatao 491 wa mwaka 2013 ambao walishaajiriwabadala ya wahitimu wa mwaka 2014.Kutokana na sababu hiyo,orodha tajwa imesitishwa kwa muda ili kufanyiwa marekebisho na kuwekwa orodha sahihi itakayojumuisha wahitimuwa SEKUCO wa mwaka 2014.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kasoro hiyo.
Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU -TAWALA ZA MIKOANA SERIKALI ZA MITAA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment