-->

MAKAMU MWENYIKITI BAVICHA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

Makamu Mwenyekiti Bavicha Taifa Patrick Ole Sosopi anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo Cha Polisi Mjini kati kwa mahojiano baada ya Maagizo kutoka ngazi za juu .
Ifahamike kwamba Ole Sosopi pamoja na Makamanda wa CHADEMA wako jimbo la Isimani Mkoani Iringa kwa ziara ya siku 28 almaarifu " OPARESHENI DELETE CCM JIMBO LA ISIMANI" ambayo leo ilikuwa inaingia siku ya 16. Katika Ziara hiyo ambayo imekuwa tishio kwa Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi na Makazi Mh, William V. Lukuvi kutokana na elimu ya Uraia inayotolewa na Viongozi hao wa BAVICHA na kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Isimani ndiyo sababu kubwa ya Sosopi kushikiliwa mpaka sasa.
Jimbo la Isimani linashikiliwa na Mh, Lukuvi kwa mda mrefu (miaka 20 sasa ) na mara nyingi amekuwa akipita bila kupinga kwa hivyo ni rahisi kusema "hajawahi kupata Upinzani kama anavyofanya Ole Sosopi " . Pamoja na utajiri mkubwa uliopo Isimani kama vili ardhi yenye rutuba kwa Kilimo na Hifadhi kubwa ya RUAHA National Park bado wananchi wamenasa kwenye tope la Umaskini wa kutumbukia . Hali hii ya Umaskini unaotajwa Isimani inatajwa kuwa ndio nguzo na kete muhimu ambayo humfanya Lukuvi kugawa lita 2 za Mahindi na Ulanzi (Pombe maarufu Iringa) na kujiapatia nafasi ya kuendelea kuwa Mbunge.
Kwa mujibu wa habari za awali kabla ya Sosopi kushikiliwa na Polisi kwa mahojiano ambayo mpaka sasa yanaendelea namnukuu...... "Marto naingia kuhojiwa hapa ndani kwa kosa la kumkashifu mh, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh, Lukuvi jambo ambalo sijalifanya kwenye Ziara yanagu " Mwisho wa kunukuu.
Kwa mujibu wa Mlinzi wa karibu wa Sosopi bwana , Raymond Kimata anasimulia jinsi ambavyo Sosopi amekuwa muda wote akijenga hoja ambazo kitaalamu zina mu - Out smart mh, Lukuvi na kuonekana atapoteza kiti cha Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October mwaka huu ndio ......" KIINI HASA " cha Sosopi kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Maelekezo yanayotoka Ngazi ya juu !!!!!
Hitimisho , Kila mpenda mabadiliko atakubalina na mimi kua Ole Sosopi ni Kiongozi mahiri na mweledi ambaye tunamuita "BAVICHA TAIFA ICON " tumuunge mkono na ni Imani yangu kwamab katika vita hii ya Ukombozi wa pili wa Taifa letu ......we shall Over come !!!!!
SOURCE:NGARANEWS
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment