Gabon, ambayo Mwaka 2012 ilikuwa Mwenyeji mwenza na Equatorial
Guinea wa Fainali za AFCON 2012, waliwabwaga Algeria na Ghana na
kuchaguliwa kuwa Mwenyeji wa AFCON 2017.
Katika Droo ya Makundi, Tanzania imetupwa Kundi G ambalo ni gumu mno kwani pia zipo Egypt, Nigeria na Chad.
Mechi za Makundi zitaanza Juni Mwaka huu na Nchi 52 kati ya 54
ambazo ni Wanachama wa CAF, ukiziondoa Somalia na Eritrea, zitashiriki.
Washindi 13 wa Makundi pamoja na Washindi wa Pili Bora Wawili,
ukiondoa KUNDI I ambalo Wenyeji Gabon wameshirikishwa lakini Mechi zao
zinachukuliwa kama za Kirafiki, ndio watatinga Fainali za AFCON 2017.
DROO KAMILI YA MAKUNDI:
KUNDI A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
KUNDI B: Democratic Republic of Congo, Angola, Central African Republic, Madagascar
KUNDI C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
KUNDI D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
KUNDI E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
KUNDI G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
KUNDI H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
KUNDI I: Ivory Coast, Sudan, Sierra Leone, Gabon
0 comments :
Post a Comment