Maalim Seif awafariji wagonjwa.
Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewaombea dua wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbali mbali ili Allah awajalie nafuuu.
Maalim ameomba dua hio wakati wa ziara maalum ya kuwatembelea wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi kadhaa katika wilaya mbili za Unguja kaskazini A na B.
Wakati wa ziara hio aliweza kuwatembea jumla ya wagonjwa 10 pamoja na wafiwa kwa lengo la kuwafariji kwa kuwapo moyo na kuwataka wasikate tama wakijua kwamba yote ni kudra ya Allah (s.w)
Katika nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa hao wameleza kufurahishwa kwao na ujio wa Maalim Seif wakiamini kuwa anawajali na kuwathamini.
‘’Hakika Mwenyezimungu atakupa lenye kheri nawe’’alieleza Bwana Said Pande wa Bumbwini.
Maalim Seif amekuwa akifanya utaratibu huu wa kuwatembelea wagonjwa kipa ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhan katika visiwa vya Unguja na Pemba.

0 comments :
Post a Comment