MALAYSIA KUVILINDA VISANDUKU VYEUSI KWA HALI YOYOTE
Malaysia
inasema itabakia na visanduku vyeusi na rikodi nyengine za data kutoka
kwenye ndege yake iliyoangushwa, MH17, hadi pale timu ya kimataifa
itakapoundwa na kuikabidhi. "Timu ya Malaysia imechukuwa udhibiti wa
visanduku vyeusi, ambavyo vinaonekana kuwa na hali nzuri. Vitawekwa
kwenye ulinzi mikononi mwa Malaysia huku timu ya kimataifa ikiundwa,"
amesema Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak hivi leo akizungumzia
kukabidhiwa nchi yake visanduku hivyo na mwakilishi wa waasi wa
mashariki mwa Ukraine.
0 comments :
Post a Comment