-->

26 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAPIGANO LIBYA,US KUFUNGA UBALOZI WAKE

Habari kutoka Benghazi, kaskazini mashariki mwa Libya zinasema kuwa watu 26 wameuawa kwenye mapigano kati ya makundi hasimu yenye silaha. Habari zaidi zinasema kuwa, zaidi ya watu 40 pia wamejeruhiwa kwenye mapigano hayo. Mashuhuda wamesema milio ya risasi imesikika usiku kucha kuamkia leo Jumapili katika maeneo mbalimbali ya Benghazi. Kwingineko mapigano makali yameripotiwa tangu jana katika mji mkuu wa Libya, Tripoli kandokando ya ubalozi wa Marekani. Hali hiyo imepelekea Washington kutangaza kufunga kwa muda ubalozi huo na kuwahamishia wafanyakazi wake katika nchi jirani ya Tunisia. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema hali mbaya ya usalama hairuhusu ubalozi wake mjini Tripoli kuendelea na shughuli zake.
Itakumbukwa kuwa, mwezi Septemba mwaka 2012 balozi wa Marekani nchini Libya aliuawa pamoja na wanadiplomasia wengine mjini Benghazi baada ya ubalozi wake mdogo kushambuliwa na watu wenye silaha.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment