-->

WAKALA WA YAYA TOURE ASEMA UBAGUZI NI KIKWAZO KWA MTEJA WAKE KUSHINDA TUZO KUBWA DUNIANI

WAKALA WA TOURE ASEMA UBAGUZI UNAMUATHIRI
Wakala wa Yaya Toure amedai kuwa sababu ya kiungo huyo wa Manchester City kutoshinda tuzo zozote kubwa ni kwa sababu ya rangi yake ya ngozi.
Wakala huyo, Dmitri Seluk amesema kiungo huyo raia wa Ivory Coast angeweza kumaliza katika nafasi ya juu zaidi ya nafasi ya tatu katika tuzo za PFA na FWA za mchezaji bora wa mwaka, na pia zaidi ya nafasi ya 12 katika tuzo ya Ballon d'Or, kama angekuwa mzungu.
Luis Suarez alishinda tuzo ya PFA na FWA akifutiwa na Eden Hazard na Steven Gerrard katika kura zilizopigwa.
Seluk ameliambia gazeti la Times kuwa "kama angekuwa mzungu, asilimia 100 angeshinda moja ya tuzo hizo kubwa.
"Sitaki kusema sana kuhusu ubaguzi wa rangi au siasa katika soka, lakini hapongezwi inavyotakiwa. Yaya ameshinda mara tatu mfululizo tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, lakini ni tofauti inapokuja katika tuzo nyingine.
"Nakubaliana na Jose Mourinho aliposema kuwa mchezaji bora wa mwaka anatakiwa kutoka katika timu inayoshinda ligi. Nina mheshimu sana Luis Suarez na Gerrard, lakini alichokifanya Yaya Toure katika nafasi ya kiungo, si mara mara nyingi wachezaji wengi wanafanikisha.
"Timu gani ilikuwa bora mwaka huu? Manchester City? Nani alikuwa mchezaji wao bora? Toure. Gerrard ni mchezaji mzuri lakini Liverpool walimaliza katika nafasi ya ya pili, na Yaya kupewa nafasi ya tatu katika kura za FWA."
Cristiano Ronaldo alishinda Ballon d'Or, na kuwazidi kura Lionel Messi na Franck Ribery.
Seluk ameongeza kusema: "Amesikitishwa kidogo na hali ilivyo. Messi ni mchezaji mzuri katika historia ya soka na ninawaheshimu sana Ronaldo na Ribery. Yaya anawaheshimu wachezaji hao. Lakini ni vigumu kwa Mwafrika katika tuzo hizi. FIFA inahitaji kubadilisha kitu hapa."
Seluk pia amekataa kuhakikisha kuwa Yaya atakuwepo City msimu ujao, akisema: "Kama klabu kubwa kama PSG au Real Madrid wakipanda dau kubwa, Man City watalazimika kuamua kitakachofuata.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment