Mahakama nchini Afrika Kusini
imekataa japo kwa masharti kumwachilia aliyekuwa kiongozi wa kikosi cha
kupinga harakati za ukombozi nchini Afrika Kusini, Eugene de Kock.
Bwana De Kock tayari ametumikia kifungo cha miaka 20.Alijulikana kama 'Muovu Mkubwa' kwa mauaji na mateso aliyowafanyia wanaharakati wazalendo mapema miaka ya themanini na tisini.
Lengo lake kuu lilikuwa kuunga mkono utawala wa mzungu.
Waziri wa sheria Michael Masutha, alisema kuwa De Kock hapaswi kuachiliwa wakati huu kwani familia yake inapaswa kushauriwa mwanzo kabla ya kachiliwa kwake.
Ila anasema De Kock amebadili tabia.
Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 65, alikamatwa mwaka 1994. Aliwahi kutoa ushahidi katika tume ya ukweli na maridhiano ya Afrika Kusini na kusamehewa kwa baadhi ya makosa ya kisiasa aliyoyafanya
0 comments :
Post a Comment