-->

IJUE SABABU YA UGOMVI KATI YA ISRAEL NA PALESTINA

SABABU ZA MZOZO WA GAZA KWA UFUPI
Ukanda wa Gaza, ni kipande cha ardhi kilichopo katikati ya Israel na Misri, na eneo hilo limekuwa kitovu cha mzozo kati ya Israel na Palestina kwa miaka na mikaka.
Israel iliikalia na kuidhibiti Gaza wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967, na iliachilia eneo hilo kwa kuondoa majeshi yake na walowezi mwaka 2005.
Israel iliona hatua hiyo kama kumaliza kuikalia kimabavu Gaza, lakini bado inaendelea kudhibiti mipaka ya Gaza, inaendelea kudhibiti mfumo wake wa maji, na pia inadhibiti anga ya Gaza. Misri inadhibiti mpaka wa Gaza upande wa kusini.
Israel iliweka sheria kali kwa watu na bidhaa kuingia na kutoka Gaza, hatua ambayo Israel inasema ni muhimu kwa usalama wake.
Hata hivyo Wapalestina wanahisi kubanwa na kufungwa, na wanaathirika na matatizo na kijamii na kiuchumi. Makundi makuu ya wanaharakati ya Palestina, likiwemo kundi la Hamas wanasema hali ya udhibiti haivumiliki.
Msimamo mkali wa Hamas ni kuiteketeza Israel, ingawa katika miaka ya hivi karibuni imesema inafikiria kuwa na makubaliano ya amani na Israel ya muda mrefu. Hamas inasema Israel kuendelea kukalia kimabavu maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki ndio sababu ya kufanya mashambulio dhidi ya Israel, kabla na baada ya 2005.
Inasema inafanya hivyo kujikinga dhidi ya mashambulio ya anga, uvamizi na mashambulio mengine ya kijeshi.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment