Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiwasili kwenye maonesho ya 38
ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja
vya maonesho vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Mwandishi wetu
Mstahiki
Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ameipongeza makampuni
yaliyochini ya Kundi la METL kwa kuhakikisha ajira kwa watanzania na
soko la mali ghafi kwa wakulima wa bidhaa mbalimbali nchini.
Silaa
alisema hayo jana wakati alipotembelea banda la METL na kujionea bidhaa
mbalimbali zinazozalishwa na makampuni yake mbalimbali zikiwemo bidhaa
za michikichi na katani.
Alisema
kwa kutengeneza sabuni, mafuta na mali ghafi nyingine kutokana na
michikichi kampuni za Metl zinawezesha wakulima kujiendeleza na pia kuwa
na uhakika wa soko.
METL
yenye makampuni zaidi ya 25 sehemu kubwa ya bidhaa zake zinatokana na
mali ghafi inayozalishwa nchini na nyingine ni zile zinazotumika kwa
ajili ya wakulima kama matrekta.
Aidha
katika banda hilo kubwa ambapo kulijaa aina mbalimbali ya bidhaa
kuanzia Sabuni,Vitenge, mafuta ya Mawese,vinywaji baridi, Matrekta na
bidhaa za nyumbani, Mstahiki meya huyo alichezesha bahati nasibu za watu
waliotembelea banda hilo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni
kwenye ofisi za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania, TANTRADE kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba mara baada ya
kuwasili.
Akizungumzia
uwekezaji wa METL, Silaa alisema kwamba anafarijika na jinsi bidhaa za
kampuni hizo zinavyoimarika ubora kila mwaka na kusema wakati umefika
kwa serikali kuangalia wawekezaji wazawa.
Alisema
kwa maoni yake serikali ione jinsi ya kuwasaidia wawekezaji wanaoagiza
mitambo toka nje ili kodi wanaoyotakiwa kulipa wailipe baada ya kuanza
kazi za uzalishaji.
“Hii
itasaidia sana kuwa na wawekezaji wa ndani ambao wataweza kutoa huduma
kama soko la mali ghjafi na pia kuongeza thamani ya bidhaa zinazoalishwa
kutoka Tanzania” alisema silaa.
Aidha
Silaa alipongeza MeTL Group kwa kuweza kutoa ajira kwa watanzania
wazawa huku bidhaa zake nyingi zikiwa kimbilio la watanzania wote, hasa
wa kipato cha chini.
Afisa
Mwandamizi wa TANTRADE, Fidelis Mugenye, (kushoto)
akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ratiba ya
ziara kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho ya Sabasaba yanayokaribia
kufikia ukingoni.
“Naipongeza
MeTL Group, kwa kuzalisha bidhaa bora ambazo ni kimbilio la wananchi
wengi… hasa bidhaa zake za mafuta, sabuni, unga, vinywaji na bidhaa
zingine kibao” alisema Silaa
Pia
aliipongeza MeTL kwa upande wa kutoa ajira na kukuza uchumi hapa
nchini, ikiwemo kuzalisha bidhaa nyingi na zenye ubora ikiwemo za kamba
ya mkonge ambayo alisema ni majibu ya utunzaji wa mazingira kutokana na
vifungashio vya plastiki kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.
Katika
bahati nasibu iliyochezeshwa mkazi wa Kijitonyama Jijiji Dar es Salaam,
Irene Manamba amejishindia zawadi ya pikipiki mpya.
Aidha,
katika droo hiyo, washindi wengine waliojishindia zawadi mbalimbali
katika droo hiyo majina yao na wanakotoka ni Victoria Charles ambaye
alikuwa mshindi wa pili mkazi wa Temeke, Julius Kamele (Tabata), Irene
Mushi (Kijitonyama), Semi Anderson ((Dar es Salaam), Happyness
Kalokola (Kitunda), Noel Kalenga (Sinza Kumekucha), Adam Mkwaya
(Mabibo), Mery Msangi (Dar es Salaam) na Aisha Abeid (Tabata).
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akisalimiana
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ndani ya ofisi
za Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania,
TANTRADE.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akiongozwa na vijana
wa skauti kuelekea kwenye mabanda mbalimbali huku akiwa ameambatana na
msaidizi wake Anthony William (kushoto).
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akipata maelezo ya
sabuni mpya ya MO BEAUTY kutoka kwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa
MeTL Group, Kelvin Msangi (kushoto) mara baada ya kuwasili katika banda
hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam
yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya
Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw.
Aunali Bandali.
Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali akimuonyesha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaabaadhi
za Vitenge na Khanga (hazipo pichani) vinavyozalishwa na kiwanda cha
21st CENTURY Textile Ltd chini ya MeTL GROUP alipotembelea banda la
kampuni hiyo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu J.K.
Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Mgeni
rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kushoto)
akipewe maelezo ya ladha za aina tofauti za soda zinazotengenezwa na
kampuni hiyo kutoka kwa Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group,
Kelvin Msangi (wa pili kulia) kabla ya droo maalum kwa wateja
wanaotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K.
Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja
Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akipata maelezo ya sabuni mbali
mbali za unga kutoka kwa Mfanyakazi wa Royal Soap Detergent Industries,
Aneth Masesa alipotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja
vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) akipata
maelezo ya aina tofauti za kamba na magunia yanayotengenezwa na kampuni
hiyo kutoka kwa Mtaalamu wa Mkonge wa MeTL GROUP, Bw. Iddi Omari (wa
kwanza kulia) wakati alipotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho
ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es
Salaam.
Msimamizi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Mrisho Millao (kushoto)
akichanganya boksi lenye majina ya wateja waliotembelea Banda la kampuni
ya MeTL GROUP na kujaza kuponi za kushiriki kwenye droo ya Bahati
nasibu ambayo imechezeshwa jana kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia), Meneja
Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) na Msaidizi wa
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi (wa pili
kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
Mgeni
rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, akichagua kuponi
ya mshindi wa kwanza kwenye droo kubwa ya Kampuni ya MeTL GROUP kwa
wateja waliokuwa wanatembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya
38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali na
Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group,
Kelvin Msangi.
Mgeni
rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kulia)
akimtangaza mshindi wa droo maalum kwa wateja wanaotembelea banda la
MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar-es-salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere,
barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Na Mshindi huyo ameshinda Zawadi
ya Pikipiki aina ya A1 ambayo imesajiliwa na seti mbili ya Vitenge,Wa
kwanza kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu Bwana
Mrisho Millao.Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi na Meneja Masoko wa MeTL Group,
Bw. Aunali Bandali (wa Kwanza kulia).
Msaidizi
wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna washindi kumi
waliopatikana watakavyochukua zawadi zao mara baada ya kupigiwa simu na
wahusika kwa ajili ya kukabidhiwa zawadi hizo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati) akipokea zawadi ya soda za MO Cola kutoka kwa Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Kelvin Msangi.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiondoka kwenye banda la MeTL
GROUP mara baada ya kumaliza shughuli ya kuchezesha droo ya bahati
nasibu kwa wateja wanaotembelea banda la MeTL Group kwenye maonesho
hayo.
Mtaalamu
wa kutembea juu kamba nchini Hassan Mkenjula a.k.a SPIDERMAN akitoa
burudani ya kupiga danadana kwa kutumia mdomo kwenye banda la MeTL
GROUP.
0 comments :
Post a Comment