LUIZ
Felipe Scolari amesema hatajiuzulu katika nafasi yake ya ukocha wa timu
ya taifa ya Brazil, licha ya timu yake kufungwa mara ya pili mfululizo
ndani ya siku tano.
Brazil
walifungwa mabao 7-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Belo
Horizonte siku ya jumanne ya wiki hii na usiku wa jana walifungwa mabao
3-0 na Uholanzi na kumaliza katika nafasi ya nne ya fainali za 2014 za
kombe la dunia kwenye ardhi yake.
Kabla
ya mashindano haya, Brazil ilikuwa haijapoteza mechi nyingi za
nyumbanii tangu mwaka 2002 na walikuwa hawajawahi kufungwa nyumbani
katika mashindo ya mpira wa miguu tangu mwaka 1975, lakini kufungwa mara
mbili mfululizo ndani ya siku tano kumewachangaya mashabiki na
waandishi wa habari wan chi hiyo.
Lakini
Scorali alikutana na waandishi wa habari baada ya kufungwa na Uholanzi
na kusisitiza kuwa shirikisho la soka nchini Mbrazil litaamua hatima
yake ya baadaye.
“Ulikuwa
mchezo wenye nguvu sawa,” alisema. “Wachezaji wanatakiwa kupongezwa kwa
jinsi walivyocheza. Hatukucheza vibaya-hayo ndio maoni yangu”.
“Kwasasa
sio muda muafaka wa kuzungumzia hilo, “ alisema Scolari. “Nitaandika
ripoti yangu na kumwambia rais wa CBF ni kitu gani nadhani hakikwenda
sawa, yeye ataamua nini anataka kwa baadaye. Tumepoteza mechi nyingine,
lakini maisha yanaendele”.
“Mwaka
mmoja uliopita nilishinda kombe la mabara,” aliongeza. “Makosa hayako
kwa makocha. Kitu ni kwamba tuna timu ya vijana sana. Hatujazalisha
wachezaji wa kutosha, kwahiyo sio kazi rahisi hata kama Kocha mwinine
atakuja”.
0 comments :
Post a Comment