-->

FAIDA 10(KUMI) AMBAZO MVUTA SIGARA HUZIPATA ANAPOACHA KUVUTA

WAJUA NINI HUTOKEA BAADA YA KUACHA KUVUTA SIGARA? TAZAMA HATUA HIZI KUMI
Unafikiria kuacha sigara? ….Yees! wazo zuri. Kwanini? Kwa sababu utaanza kuona faida za kuacha kuvuta sigara ndani ya dakika ishirini tu baada ya kuacha! Wajua inachukua muda gani mpaka kiasi cha nicotine kutoka mwilini mwako? Soma haya…

1.Dakika ishirini (20) tu, baada ya kuacha kuvuta sigara mapigo yako ya moyo huanza kurudi katika hali ya kawaida

2. Masaa mawili baada ya kuacha kuvuta sigara, mzunguko wako wa damu hurudi katika hali ya kawaida. Kiwango cha nicotine hushuka mpaka asilimia 6.2

3. Wajua wavuta sigara wana hasira za haraka? Baada tu ya masaa 24 yaani siku moja baada ya kuacha sigara, mvutaji hujisikia mwenye amani na akikaa hivyo kwa wiki moja zaidi hujisikia katika hali bora zaidi.

4. baada ya siku mbili tu toka uache kuvuta sigara, neva zilizoanza kufa huanza kurudi katika hali yake na kiwango cha kunusa na uwezo wa ulimi kutambua ladha huongezeka!

5. Siku tatu baadae mwili wako hautajisikia kuwa na nicotine tena kwa asilimia 100% japo bado itakuwepo kwa kiasi Fulani. Na utaanza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama TB au mshtuko wa moyo.

6. Wiki moja tu baada ya kuacha sigara utakuwa na uwezo wa kufanya shughuli yoyote ya kutumia nguvu ambayo mwanzo ulikuwa ukichoka kwa haraka baada tu ya kufanya hivyo.

7. Mwezi mmoja mpaka mitatu baada ya kuacha, mapafu yako huanza kuwa safi na kurudi katika hali yake ya kawaida

8. Mwaka mmoja baada ya kuacha sigara, hatari yako kupata magonjwa kama TB na mshtuko wa moja hushuka mpaka asilimia 50% kulinganisha na mvutaji!

9. Miaka mitano baada ya kuacha sigara Utakuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata kiharusi. Na kupunguza kama si kuondoa kabisa uwezekano wa kupata TB (inategemeana umevuta kwa mda gani)

10. Miaka Kumi na zaidi baada ya kuacha sigara, tapunguza uwezekano wa kupata kansa ya mapafu, na madhara hayataonekana mwilini mwako kwa asilimia karibu mia moja (100%) na Utakuwa na furaha zaidi maishani.

CREDIT TO FADHILI PAULO ==>bit.ly/VEpd5E
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment