-->

PAPA FRANCIS AWAAOMBA WAPALESTINA NA WAISRAEL KUSITISHAA MAPAMBANO

 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, leo amezungumza kwa simu na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina na Rais Shimon Peres wa Israel akiwatolea wito wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. Papa Francis amewakumbusha viongozi hao wawili haja ya kukomesha uhasama, kufanya juhudi za kupatikana amani na muafaka kwenye nyoyo za wale wanaohusika na kadhia hiyo. Taarifa ya makao ya Kanisa Katoliki, Vatican, iliyotolewa leo inasema "Baba Mtakatifu anawazingatia Abbas na Peres kuwa ni watu wa amani na wanaosaka amani."
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment