Argentina na Ujerumani zitachuana kwa mara ya 3 katika fainali ya kombe la dunia.
Je wajua itakuwa mara ya 8 kwa timu hizo kuchuana katika kombe la dunia ?Ukinzani wa jadi kati ya Brazil-Argentina unaweza kumithilishwa tu na uhasama baina ya Ujerumani na Uholanzi.
Lakini baada ya Argentina kutinga fainali ya kombe la dunia huko Brazil dhidi ya Ujerumani Uhasama wa kikanda baina ya Argentina na Brazil umeibuka upya.
Mashabiki wa Brazil wanaona kheri kushabiki Ujerumani iliyowaadhibu mabao 7-1 kuliko kuitizama timu wanayoichukia zaidi Argentina ikitazwa mabingwa wa kombe la dunia mwaka wa 2014 nchini Brazil,,ni kama msumari kwenye kidonda anasema Sanche raiya wa Brazil.
Maoni yake yanafanana na maelfu kama si mamilioni ya wa Brazil .
Argentina itakuwa inakutana na Ujerumani kwa mara ya tatu katika fainali ya kombe la dunia ambayo ni rekodi mpya baina ya mahasimu hao wawili.
1958
Wajerumani wakiwa ndio mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani waliibuka washindi mabao win 3-1.
1966
Ujerumani ilitoka sare tasa na Argentina katika mechi za mkondo wa kwanza .
1986 Fainali
Argentina iliibuka washindi kwa mabao 3-2 .
Huu ndio mwaka ambao Mshambulizi wa Argentina Diego Maradona alifunga kwa mkono timu hizo zilipokuwa zimetoshana nguvu 2-2 hadi katika dakika ya 84 ya kipindi cha pili.
1990 Fainali
UJerumani iliibuka washindi kwa bao moja kwa nunge kupitia penalti ya dakika ya 85 katika kipindi cha pili.
2006 (Robo fainali)
Argentina walikuwa wamewadhibiti wenyeji wao huko Berlin mechi hiyo ilipokamilika 1-1 katika muda wa ziada .
Die Mannschaft walijifurukuta na kuilaza Argentina 4-2 kupitia mikwaju ya penalti.(Ujerumani hatimaye ilishindwa na Italia katika nusu fainali)
2010 (Robo fainali)
Hii ndilo lililokuwa kombe la dunia la kwanza kuandaliwa katika bara la Afrika na mahasimu hao walikutana katika hatua ya robo fainali Argentina ikifunzwa na nyota wao Maradona.
Thomas Müller aliiongoza Ujerumani kuititima Argentina mabao 4-0 .
Mechi hii ndiyo iliyodhibitisha Thomas Müller na Miroslav Kose ni wa shambulizi wenye haiba ya juu.
Kuanzia wakati huo Argentina wamekipika kikosi chao upya sasa wakimtumia nyota wao Messi kama mshambulizi wa pekee.
Hiyo yote ni Historia je Jumapili ni nani atakayeibuka mshindi ?
Ujerumani ambayo kila mchezaji anauwezo wa kufunga mabao ama Argentina yenye uwezo mkubwa lakini ikimtegemea Messi kuifikisha kwenye Fainali ?
BBC SWAHILI
0 comments :
Post a Comment