-->

DONDOO ZA AFYA:UJUE UMUHIMU WA KUTEMBEA KWA MIGUU KATIKA AFYA YA BINAADAMU

Kutembea ni moja ya mazoezi yanayohimizwa kufanya na
yanayoweza kusaidia kujenga afya ya mwili.

Miongoni mwa mazoezi mepesi na yasiyo na masharti makubwa ni
yale ya kutembea. Kutembea ni njia rahisi za kufanya mazoezi.
Mtindo wa maisha unawafanya wengi kutumia magari au usafiri
wa aina nyingine hata katika eneo la umbali mfupi.


Kama wazee wetu walivyoishi kwa kutembea hata sisi tunajionea jinsi walivyo wakakamavu na walivyoishi muda mrefu. Miongoni
mwa mazoezi mepesi na yasiyo na masharti makubwa ni yale ya
kutembea. Kutembea ni njia rahisi za kufanya mazoezi.


Huhitaji vipimo vya afya kuweza kufanya zoezi hili na badala yake
unahitaji mavazi yasiyokwaza, pamoja na mahali pa kutembelea.
Wakati wataalamu wa afya wanapendekeza kupata ushauri wa
daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi magumu, lakini mazoezi
mepesi yanashauriwa kwa mtu yeyote na mahali popote.


Wataalam wa masuala ya afya, wanasema kutembea ni njia
salama na nzuri inayosaidia kuujenga na kuuimarisha moyo
uwe na afya nzuri na usio katika hatari ya kushambuliwa na
maradhi.


Nae mtaalamu wa mazoezi katika Gym anasema mazoezi au
tabia ya kufanya mazoezi inayo faida kubwa zaidi kuliko matumizi
ya dawa. Kutembea ni moja ya mazoezi yanayohimizwa kufanya na yanayoweza kusaidia kujenga afya ya mwili.

Wataalamu wa masuala ya afya na magonjwa ya moyo wanasema
kutembea ni miongoni mwa kinga ya mwili kushambuliwa na
magonjwa mbalimbali ukiwemo wa moyo na kiharusi.


Kutembea vile vile ni tiba kwa mtu mwenye kusumbuliwa na matatizo ya ubongo na kwamba, badala ya kujenga tabia ya kutumia dawa za kupunguza msongo wa mawazo, ni
vyema mtu mwenye tatizo hilo akajenga tabia ya kutembea kwa
dakika 20-30 kila siku.


Kutembea kunazuia ugonjwa wa kisukari kutokana na mazoezi hayo kuboresha uwezo wa mwili wa kutumia tezi ya insulini.
Kutembea vilevile kunaiweka mifupa kuwa imara na kuikinga na
mashambulizi ya kuzuia ugonjwa wa mifupa. Kutembea kunasaidia
kupunguza uzito unaoongezeka bila mpangilio.


Kutembea huboresha usingizi, huchochea utendaji kazi wa
ubongo, na kumsaidia mtu asishambuliwe na maradhi ya mshtuko wa moyo. Mbali na kutembea kama zoezi, kutembea kwa starehe vilevile kunaweza kuleta faida na afya kwa mwili.

Wataalamu wa afya na mazoezi wanasema watu wanaotembea
mara kwa mara huwa na faida moja kubwa, ya uwezekano wa
kuishi muda mrefu kuliko wale wanaotumia magari kwa muda
mrefu.
Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye kujijenga tabia ya kufanya
mazoezi ya kutembea, anajiongezea nafasi ya kuwa na mwili wenye afya njema, imara na usio hatarini ya kushambuliwa na
maradhi. http://www.manyandahealthy.com
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment