-->

KIJANA MWINGINE NAE ATIWA BAKORA KWA KULA MCHANA WA RAMADHANI HUKO PEMBA




By Mazrui Media & Communication
BREKING NEWS:
kutoka https://www.facebook.com/pages/Mazrui-Media-Communication/247412001951938
APATA KIPIGO BAADA YA KULA MCHANA
WA RAMADHANI
Mtu mmoja kisiwani Pembae ambae hadi sasa bado jina lake halijafahamika amejeruhiwa vibaya baada ya kupata kipigo kutoka kwa askari jamii.

Mkasa huo umetokea katika kijiji cha Msingini Chake chake mkoa wa kusini pemba ambapo Polisi jamii wa Shehia hio waliamua kumpiga mtu huyo baada ya kuoneka akila mchana akiwa pamoja na wenzake watatu ambao wamefanikiwa kukimbia na kutokomea kusiko julikana.

Mtoa taarifa wetu akizungumza na mazui media amesema watu hao walikua ndani ya nyumba wakipika sembe na kujidunga madawa ya kulevya mchana wa leo katika shehia ya hio ya Msingini.

‘’Unajua tunawashukuru sana hawa Polisi jamii wetu wanajitahidi mno hususani kipindi hichi cha Ramadhani hatuwezi kukubali kuona watu wanakula ovyo katika kisiwa chetu’’alieleza mtoa taarifa hii ambae hakupenda jina lake litajwe.

Aidha Polisi jamii hao kwa sasa wananmfikisha mtu huyo katika kituo cha polisi Chake chake ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria zaidi.

Mazrui media inafanya jitihada za mawasiliano ja Jeshi la Polisi kisiwani Humo ili kupata habari zaidi.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment