-->

PAPA FRANCIS KUKUTANA NA WALIOFANYIWA UNYAMA WA KUNAJISIWA

Papa Francis hii leo anatarajiwa kukutana kwa faragha na kundi dogo la waathiriwa wa unyanyasaji wa kimapenzi waliotendewa na mapadri wa kikatoliki. Ni mara ya kwanza kukutana na waathiriwa hao tangu achaguliwe miezi 16 iliyopita.
Papa ametaja unyanyasaji huo kama misa ya shetani na ameahidi kwamba ni jambo lisilo kubalika hata kidogo.
Kanisa katoliki huko Vatican - ambalo liaendelea kuficha rekodi zake kuhusu mapadri waliowanyanyasa watoto, lina sita kutoa taarifa zozote kuhusu mkutano huu kabla ufanyike.
Lakini inafahamika kwamba wanawake na wanaume walioathiriwa kutoka Ireland, Uingereza na Ujerumani, watahudhuria misa ya asubuhi alafu baadaye watakutana na Papa faraghani.
Kashfa hiyo iliyozushwa kutokana na ufichuzi wa muongo uliopita wa kuenea kwa unyanyasaji dhidi ya watoto katika nchi nyingi, hususan wa miaka mingi ya nyuma - umeathiri imani kwa kanisa hilo.
Papa Francis sasa ameunda kamati ya wataalamu, wanawake na wanaume, wakiwemo madakatari wa magonjwa ya akili, viongozi wa dini na muathiriwa mmoja.
Marie Collins kutoka Ireland, kufanya mipango ya kukabiliana na mapadri wa aina hiyo.
Marie Collins alinyanyaswa kimapenzi na mhudumu wa hospitali akiwa na miaka 13 na sasa anashinikiza kampeni kwa niaba ya waathiriwa.
Na kadinali Sean O'Malley ambay ni askofu wa Boston ambako mzozo huo wa unyanyasaji wa kimapenzi ulizuka kwanza Marekani, pia ni mwanachama.CHANZO BBC,(A.I).
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment