picha ya majeruhi wa kuangukiwa na kifusi
picha ya mmoja ya mwili wa marehemu uliofanikiwa kupatikana
Kwa hisani ya Mussa Juma na Moses Mashalla, Mwananchi na Global publishers
Arusha. Siku tatu baada ya ghorofa kuanguka na kuua watu 36 jijini Dar es Salaam, maafa mengine yametokea jana mkoani Arusha ambako watu wapatao 20 wanahofiwa kufa baada ya kufunikwa na kifusi cha `moramu’ wakati wakifanya shughuli za uchimbaji eneo la Moshono, Arusha.
Maiti
za watu 14 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa hadi jana jioni wakati watu
wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na kukimbizwa katika
Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na kuvunjika miguu.
Waliotolewa
wakiwa hai walitambuliwa kuwa ni Matei Nenano na Lushooki Laizer wote
wakazi wa jijini Arusha. Mwananchi lilishuhudia vikosi vya uokoaji
kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi pamoja na wananchi
wakitoa msaada wa kufukua kifusi hicho kwa ajili ya kutoa watu
waliofunikwa.
Maiti zilizoopolewa ni za mmiliki wa
magari ya kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald
Lutakata, Hassan Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu
Ruafela.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.
Watu
walioshuhudia tukio na taarifa hizo kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha, Hemed Kilonge walisema lilitokea jana saa 5.00
asubuhi wakati shughuli za uchimbaji zikiendelea.
Kamanda
Kilonge alisema wakati wachimbaji hao wakiwa ndani ya shimo wakiendelea
na kuchimba ‘moramu’, ghafla gema liliporomoka na kuwafunika
0 comments :
Post a Comment