Mahakama Kuu Kenya yasema Uhuru alichaguliwa kihalali
Mahakama kuu ya Kenya imetangaza muda mfupi uliopita kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali katika uchaguzi mkuu uliopita Kenya. Uamuzi huo unakuja wiki kadhaa baada ya uchaguzi kufuatia hatua ya mpinzani wake Raila Odinga kupinga matokeo hayo na kufungua madai mahakama kuu. Leo mahakama kuu inasema uchaguzi ulikuwa huru na halali.
Wakenya wamekuwa wakisubiri uamuzi wa mahakama kwa shauku kubwa. Polisi Ijumaa ilitoa ilani kwa wafuasi wa pande zote mbili kujiepusha na kushereheka au kulalamika kufuatia uamuzi wa mahakama.
Kulingana na ratiba Uhuru Kenyatta ataapishwa rasmi kuchukua uongozi wa Kenya Aprili 9, 2013
kwa ihsani ya http://zanzibarislamicnews.wordpress.com/2013/03/30/mahakama-kuu-kenya-yasema-uhuru-alichaguliwa-kihalali/
0 comments :
Post a Comment