-->

SHIDA YA MAJI YA ZAIDI MKOANI MOROGORO


Katika hali isiyoyakawaida mkoa wenye neema ya vyanzo vya maji umeendelea kuimba wimbo wa shida ya maji pamoja na mvua nyingi zinazo nyesha lakini kwa mkoani Morogoro hiyo haujawa sababu ya kufuta shida ya maji kama ilivyotegemewa na wananchi wengi.
Mkoa wa Morogoro unavyanzo vingi vya maji ila vyanzo vikuu vya kunywesha maji Morogoro mjini na baadhi ya sehemu ya Morogoro vijijini ni bwawa la Mindu ambalo hutoa huduma maeneo ya Chamwino,Mafiga,K/Ndege,Mjimpya,Mawenzi,Ujenzi,Mazimbu,Kasanga, na maeneo mengine,Pia  maji hutoka mlima wa Uluguru ambayo hutoa huduma yamaji kwa  maeneo ya Mjimkuu,Bomarodi,Uhuru,Vibandani,SUA na maeneo mengineyo.
Wananchi wamekosa taarifa za msingi kuhusu tatizo hilo la maji ambalo ambalo lilitegewa kuelezwa kwa kina na kufafanuliwa na John Mtaita ambaye ni kiongozi wa MOROWASCO(Idara ya maji safi na maji taka mkoani Morogoro) kwani mara nyingine maji hutoka machafu na kunuka kama vile mzoga.Maji hayo huwa ni machafu na kuwa na rangi ambayo huogopesha kuyanywa kutokana na rangi yake na matakataka yanayokuja nayo.Kwa muonekano maji hayo hutishia hata kuoga kwani watu huogepea kupata magonjwaa kama kichocho,fangasi pamoja na magonjwa mengine yanayosambaa kupitia njia ya maji.
Pamoja na hayo lakini maji yalikuwa yakipatikana kwa muda lakini kwa sasa yanatoka usiku wa manane tena kidogo na muda mwingine huchukua siku kadhaa pasina kutoka kabisa.
Blog hii inatoa ushauri kwa idara ya maji safi na maji taka kuboresha miundombinu ili huduma ya maji kwa wateja wao iweze kuboreshwa,Pia blog hii intoa ushauri kwa idara ya maji kutoa taarifa ya sababu za msingi ya kukatika kwa maji kabla hayajakatika ili wateja wao wajiandae na tatizo.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment