-->

MANCHESTER UNITED YATANGAZA UBINGWA IKIWA BADO MECHI NNE

Timu ya Manchester United ilifanikiwa kumtandika Astonvilla katika uwanja wa Old traford,mechi ambayo ilishuhudiwa na mashabiki zaidi ya elfu sabini na tano.Robin vanpersie alikuwa wa kwanza kufungua milango ya nyavu za Astonvilla na kisha kuendelea kwa kutandika bao la pili ambalo limetajwa na wahandishi wa habari kuwa ni huenda likawa bao bora la msimu mzima.bao hilo lina fanana sana na bao ambalo alishawahi kufunga akiwa Arsenal akipokea pasi kutoka Alexanda Song.Kisha Robin vernpersie alifunga kitabu cha magoli kwa kupiga bao la tatu na la mwishi kwenye mchezo huo.Baada ya muda mrefu kucheza pasina mafaniko hatimae Robin vanpersie amefanikiwa atafanikiwa kunyanyua kombe akiwa na mashetani hao wekundu.
Timu ya Manchester united imebakisha mechi nne ili imalize ligi lakini tayari imekwisha tangaza ubingwa rasmi katika mchezo huo uliopigwa dhidi ya Astonvilla.Kazi iliyopo mbele ya Fergie ni kuhakikisha timu inaweka rekodi ya kuchukua kombe ikiwa na pointi za ya 95 ambazo ziliwekwa na Chelsea.
Hapo chini ni picha matukio ya uwanjani na baada ya mechi ya hiyo








Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment