Na Ibrahim Yamola, Dar es Salaam.
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.
Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo
2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la
saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi
ya chuo kikuu.
Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na
Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani
mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu
kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya
kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu,
lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha
mitihani hiyo maalumu.
Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama
‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa
vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.
“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya
Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk
Maronga na kuongeza:
“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini
wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa
habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo
bila tatizo.”
Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.
Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni
75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja
E ni 0-34.
“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa
kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa
kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha
kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.
Alibainisha kuwa mitihani itakayokuwa ikitumika kudahili
watahiniwa itakuwa ni wa somo la Kiingereza na Hisabati utakaokuwa na
alama 30.
Mtihani wa Pili utakuwa na alama 30 ambao ni
mtihani wa Maarifa na wa tatu utakuwa na alama 40, utakaokuwa ukitokana
na fani husika ya mwombaji.
“Mfano mtahimiwa anataka kusomea sheria au
uandishi wa habari, atatakiwa kufaulu kwa asilimia 50 somo husika, hivyo
endapo atakosa kupata asilimia 50 ya somo lake hatapata cheti
kitakachomwezesha kuendelea na elimu ya juu,”alisema Dk Marango na
kuongeza:
“Cheti tutakachompatia mtahiniwa kitakuwa halali
kwa kipindi cha miaka mitatu na baada ya hapo mwombaji atatakiwa kufanya
upya mitihani hiyo.”
Viambatanisho
Kutokana na maelezo ya TCU, mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria,wasifu wake pamoja na vyeti vya ushiriki mzuri kutoka sehemu anayofanyia kazi.
Kutokana na maelezo ya TCU, mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria,wasifu wake pamoja na vyeti vya ushiriki mzuri kutoka sehemu anayofanyia kazi.
Vingine ni nakala za vyeti vya taaluma, picha
ndogo ‘passport size, nakala za vyeti vya taaluma za masomo ya hapo
awali, ripoti ya tathmini ya utendaji kazi wake kazini kwa walioajiriwa
kutoka kwa mwajiri na nakala ya kozi za awali alizokwishafanya.
Vituo vya Mitihani
Mkurugenzi huyo alisema mitihani itafanyika kati ya Mei na Juni mwaka huu katika vituo vinne vilivyoandaliwa katika vyuo.
Mkurugenzi huyo alisema mitihani itafanyika kati ya Mei na Juni mwaka huu katika vituo vinne vilivyoandaliwa katika vyuo.
Alisema kuwa chini ya mfumo huo Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), kitahusika na masuala ya Elimu huku Chuo Kikuu Tumaini
Makumira cha Dar es Salaam (TUMADARCo) kikihusika na Uandishi wa Habari
na Mawasiliano kwa Umma.
Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), kitahusika na
Kilimo na Wanyamapori wakati Chuo Kikuu cha Mzumbe (MU) kitahusika na
masuala ya usimamizi na utawala,uhasibu, sheria na Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (ICT).
“Kwa kuwa ndiyo tunaanza, tumeamua kutenga vituo
vinne, lakini mwakani tunatarajia kuongeza viwe vingi ili kukidhi
mahitaji ya wananchi walio wengi,”anasema Dk Marongasource mwananchisoma zaidi
0 comments :
Post a Comment