BARCA WAGEUZWA BUCHA NA BUYERN
Timu ya Barcelona ambayo imekuwa ikisadikika kwamba ni miongoni mwa timu bora Duniani,leo hii imepata kipigo cha bao 4 kwa 0.Muller aliazisha kipigo hicho mwanzoni tu mwa mchezo baada ya kuwatandika goli la kichwa na kisha kufuatiwa na Gomez kwa kutandika goli la pili.Wakati Barca wamepanic na kutaka kurejesha magoli ndipo walipojikuta wanahari mbaya zaidi kwani Roben aligeuza mabeki wa Barcelona na kufanya anachotaka kwa kuwapiga bao la tatu.Mambo hayakuishia hapo kwani Timu ya Buyern munich walikuja juu zaidi na kutawashambulia Barcelona kama nyuki na kupelekea kupata goli la nne kupitia mchezaji wao aitwae Muller ambae lilikuwa bao la pili katika mchezo huo.
Mchezaji mkali wa Barcelon Lionel Messi ameshindwa kutamba katika mchezo huo na kufanya timu zima kuzorota kwani timu hiyo imekuwa ikimtegea kupita kiasi.Hivy kupotea kwake ndo kupotea kwa timu hiyo.
Katika mchezo huo mchezaji wa Barcelona Gerard Pique alishika mpira ndani ya kumi na nane mara mbili na refa alipeta kwa kutokujali hilo.
0 comments :
Post a Comment