Robert Lewandowski mchezaji wa timu ya Dortmund ambae ni raia wa Poland jana usiku aliwafanya vibaya Real madrid kwa kuwatandika bao nne mguuni mwake huku Madrid wakimbulia bao moja tu kupitia mshambuliaji wao mkali aitwae C.Ronaldo na baada ya goli ilo mchezaji alishindwa kutamba kwani ilikuwa ni dhamu ya Lewandowski kuwafundisha mpira mabeki wa Real madrid.Lewandowski alitandika mabao yake katika dakika ya 8,50,55 nq 60.
Lewandowski kwa sasa ana bao 12 sanjari na C.Ronaldo ambae nae pia anabao 12 na kufanya upinzani huo wa nani ataongoza kwa magoli katika klabu bingwa ulaya kuwa ni tata.Inaaminika kwamba mechi itayochezwa nchini Hispania ndiyo itakayoamua nani atabeba kiatu cha dhahabu.
Lewandowski akionyesha kwa ishara ya mikono kwamba amewapiga bao nne Real madrid
0 comments :
Post a Comment