Picha ya kibonzo hicho iliyopo ukurasa mbele wa gazeti hilo inamwonyesha Mtume Mohammad akilia.
Wandishi wa jarida la Charlie Hebdo wamechapisha picha ya kibonzo cha mtume Muhammad
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa picha hiyo itachochea chuki.
Hata hivyo waandishi wa habari wa gazeti hilo wanasema ukurasa wa mbele unamaanisha Waandishi wa habari wamewasamehe waliotekeleza shambulizi la kigaidi lilolofanyika jumatano wiki iliyopita.
Naibu Mhariri wa Gazeti la Liberalation Alexandra Schwatzbrod anasema ulikuwa uamuzi mwepesi kwa gazeti lake kuchapisha picha ya kibonzo hicho..
SOURCE:BBCSWAHILI
0 comments :
Post a Comment