1. Jali pesa yoyote uipatayo, usidharau hata shilingi mia yako maana ukiweza kutunza fedha ndogo hata kubwa utafanikiwa kuitunza
2. Jenga mazoea ya kufikiria mawazo tofauti ya biashara hata kama hujawa na mtaji, ili ukipata mtaji uanze biashara moja kwa moja
3. Mbali na kuajiriwa pia kuwa na fikira za kuanzisha biashara ndogo ndogo utakazoweka mtu kuzisimamia ili siku ukiishia fedha ya kutumia zile biashara zikusaidie.
4. Hakikisha kila fedha uipatayo unaweka akiba yake maana unaambiwa 'Haba na haba hujaza kibaba'
5. Usipende kuwa na matumizi yasiyo na lazima sana, kama unaona bajeti yako haitoshi kufanya matumizi ya milioni moja usijilazimishe , fanya yale matumizi uliyo na uwezo nayo na usiiishi kwa kumuiga fulani.
6. Changamkia kila fursa unayoipata katika kufikisha malengo yako, ukipata fursa ya kusoma nenda, ukipata fursa ya biashara fanya, maana ukiacha fursa zipite utazijitua baadaye.
7. Ishi vizuri na watu maana watu wakuzungukao ndio wanaweza kufanya wewe ukafikia malengo uliyonayo maana kila mtu anapotaka kufanya kitu atakufikiria wewe ila ukijifanya mjanja nao watakutosa.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment