Hapo jana katika mitandao mbali mbali ya kijamii ziliibuka taarifa kwamba Mwigulu Nchemba amepotea angani na Helkopta kwa masaa 6 na mwenyewe alithibitisha kupotea huko akiwa Tanga(bofya hapa kuisoma habari hiyo) kupitia akaunti yake ya faceboo Mwigulu Nchemba amekanusha taarifa na kusema kwamba ni uzushi
"Watanzania,
Kwanza napenda kuwashukuru kwa kuendelea Kuniunga mkono na Kuniombea katika kazi Zangu.
Pili,Napenda kukanusha kwa kile kinachoenezwa kuwa "Mwigulu apotea angani kwa Masaa Sita"
Hii ni habari ya Uongo,Uzushi ambayo ama kwa Maksudi au kwa kuwa na uelewa mdogowameamua kuiandika Mitandaoni na kuisambaza kwenye vyanzo mbalimbali vya habari.
Kwanza tambueni ukweli huu,
1.Helkopta ikijazwa Mafuta "Full" inauwezo wa kukaa Angani kwa Masaa yasiyozidi Matatu(3) angani kabla haijajazwa tena.Hivyo hayo masaa sita wanayodai tulipotea ni dhahili hawakujipa fursa ya kuelewa Helkopta inakaangani kwa muda gani ikiwa na Mafuta Full.
2.Jana nimefanya ziara ya Kuzunguka Mkoa wote wa Tanga,Nimefanya Mikutano 8(Kilindi,Handeni,Kabuku,Panga ni,Tanga Mjini,Maramba,Muheza na Korogwe).Mkutano wangu wa kwanza nimeufanya Kilindi saa 5:20 Asubuhi.
Je,ningewezaje kufanya Mikutano yote 8 wakati nimepotea angani kwa masaa 6??
Inasikitisha kuona Muda wa Kufanya kazi za Maendeleo Unatumika
kuzalisha Habari za Uongo kama hizi,Nawatakia kazi njema na Ujenzi Mwema
wa Taifa letu.
Mwisho,Asanteni sana Wananchi wa Mkoa wote wa Morogoro kwa Mikutano yote ya leo,Mkataba wa CCM na Watanzania ni kuhamasisha na kuwaletea Maendeleo tu.
"Mabadiliko ni Vitendo"
Mwisho,Asanteni sana Wananchi wa Mkoa wote wa Morogoro kwa Mikutano yote ya leo,Mkataba wa CCM na Watanzania ni kuhamasisha na kuwaletea Maendeleo tu.
"Mabadiliko ni Vitendo"
0 comments :
Post a Comment