TETESI ZA SOKA ULAYA - DIRISHA DOGO LA USAJILI
Manchester United wamekaririwa kutaka kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 112 kumnunua beki wa kati Marquinhos, 20, kutoka Brazil anayechezea Paris St-Germain (Sun), Man Utd pia sio timu iliyotoa dau la pauni milioni 26 kumtaka beki wa Valencia Nicolas Otamendi, na huenda wakarudi kwa Mats Hummels mwisho wa msimu (Manchester Evening News), Tottenham wanataka kuwashawishi Everton kumuuza winga wao kutoka Ubelgiji Kevin Mirallas, na wako tayari kumtoa Aaron Lennon katika mkataba huo (Daily Mirror), hata hivyo Everton inaarifiwa kukataa pendekezo hilo (Sun), kiungo wa Zenit St Petersburg, Axel Witsel, 26 amesema anataka kucheza ligi kuu ya England, na Man Utd huenda wakamtaka (Bleacher Report), kiungo wa Barcelona Xavi anataka timu yake imsajili kiungo wa Arsenal Santi Cazorla, 30 (Metro) Chelsea wanataka kumsajili winga wa Fiorentina Juan Cuadrado, 26 lakini huenda wakalazimika kuwauza kwanza Andre Schurrle, 24 na Mohamed Salah, 22 (Daily Mirror), kiungo wa Manchester City, James Milner, 29, huenda akaondoka kwenda Italia au Spain kwa kuwa mazungumzo ya mkataba mpya yanasuasua (Guardian), Arsenal wameanza mazungumzo na Villarreal kuhusu kumsajili beki wa kati kutoka Brazil Gabriel Paulista, 24 (Telegraph), Crystal Palace wanataka kumsajili kiungo kutoka Cameroon Stephane Mbia, 28 anayechezea Sevilla (Daily Mail). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

0 comments :
Post a Comment