Hekaheka
ya leo January 5 inatoka Shinyanga ambapo ndugu wa mwanamke mmoja
aliyefariki walimpasua tumbo marehemu huyo na kumuwekea kifaranga cha
kuku kikiwa kizima.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa
marehemu alifariki akiwa na tatizo la uvimbe tumboni, makubaliano yao
ilikuwa kwamba wafanye shughuli hiyo wakati mwili wa marehemu akiwa
hospitali lakini mtafaruku ukazuka pale ambapo ndugu hao waliamua
kufanya zoezi hilo wakati jeneza limeshushwa ndani ya kaburi.
Watu waliamua kususia mazishi baada ya
mtu huyo ambapo ndugu wakaamua kufanya mazishi hayo wenyewe ambapo
Polisi waliingilia kati pia kujua chanzo cha mtafaruku huo.
Imesemekana mzozo wa mazishi hayo
ulitokana na kijana aliyemuoa mwanamke huyo kutotoa mahari hivyo ndugu
hao wakataka wapewe pesa kiasi cha mil.2 ili waruhusu mazishi hayo
yafanyike.
0 comments :
Post a Comment