Nimefurahishwa sana na jukumu la UDASA kuonesha njia kwa masuala
ambayo yanakwamisha demokrasia ya kweli na uwazi katika uchaguzi wetu.
Lakini niseme kwamba siungi mkono utaratibu wa kufanyisha midahalo ya wagombea wa chama kimoja kimoja, halafu baadaye kuja kuwaunganisha wa vyama vyote na kuanza midahalo ya pamoja (hadi ntakapofahamishwa vizuri). Mawazo yangu ni kuwa, midahalo ikiwahusu wagombea wa vyama vyote kwa ujumla wao na wale wa binafsi kama watakuwepo.

Itabidi UDASA isubiri vyama viteue wagombea urais na ndipo iitishe
jukwaa la wagombea urais (mmoja kutoka kila chama). Midahalo ifanyike
wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu na inaweza kuwa mitatu au minne. Kama
kampeni za safari hii ni siku tisini, yaani miezi mitatu, inapasa UDASA
iite mdahalo wa kwanza mara tu NEC inapowateua wagombea hao. Kisha
mdahalo wa pili ufanyike siku ya 21, wa tatu ufanyike siku ya 42 na wa
mwisho ufanyike siku 7 kabla ya siku ya upigaji kura.
UDASA isijali hata kama chama kimoja mgombea wake atakimbia, tuliona pale Kenya, kuna wakati UHURU aliazimia kutoenda kwa midahalo, sote tuliona kabisa kuwa kwa mwelekeo wa ushindani angejiangusha mwenyewe. Uamuzi wa kuendelea na midahalo ulimpeleka mbele, akajitofautisha na wagombea wote. Raila Odinga alishindwa kuwavutia vijana wengi, kuanzia alivyokuwa akiongelea matatizo yao na hata alivyokuwa anaongea kizee. Platform ile ilimfanya Uhuru aonekane kama mtu mwenye uwezo na ufahamu mkubwa, ni mkenya wa kisasa asiyeishi ukale wa watu waliopita.
Kwa hakika, mdahalo huu wa UDASA na ITV utakuwa chachu kubwa ya mabadiliko ya kifikra na itafanya wananchi wengi wasio na tabia ya kupiga kura wajitokeze kwa sababu morali ya kuwajua wagombea itawafanya waone kumbe waongeaji wana dhamana kubwa zisizopaswa kudharauliwa.
Sioni umuhimu wa kufanya midahalo ya wagombea wa CHADEMA kwa CHADEMA, CCM kwa CCM au CUF kwa CUF na kwa mantiki hiyo nakubaliana mia kwa mia na hoja za Mwenyekiti wa kudumu Maggid Mjengwa.
Naomba sasa, Mwalimu wangu Prof. Kitila Mkumbo aje hapa atufafanulie mantiki ya kushindanisha wagombea wa kila chama peke yao ili tujadili na kuona umuhimu wa hoja hiyo, ili tutoke tukiwa kitu kimoja katika kuunga mkono jitihada za UDASA hii mpya yenye mvuto, pamoja na ITV, Televisheni ya Taifa letu.
J. Mtatiro,
Dar Es Salaam,
16 Jan 2015.

0 comments :
Post a Comment