-->

CCM WACHARUKA,SHAKA AFUKUZWA KWENYE KIKAO CHA CCM ZANZIBAR


Shein
Habari za mwaka mpya nataraji mupo salama buheri wa afya. Mtu wangu karibu zaidii amenijuza haya yaliyojiri katika Kikao cha kwanza CCM kisiwandui ambapo mwekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar Dr Shein. Kikao hichi ni kufutia vikao 2 ambavyo vimefanyika huko huko Zanzibar baada ya sherehe za Mapinduzi kuadhimishi miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo vikao hivi 2 Mwenyekiti wake alikuwa Rais Jakaya mrisho Kikwete.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimtoa nje ya ukumbi ndugu Shaka Mwenyekiti Vijana CCM Zanzibar na Rais kuagiza awe chini ya ulinzi.
Hii ilitokana na kikao hicho Baada ya Mwenyekiti wa Kikao hicho Rais Shein kuanza kutaja matarajio na tathmini ya chama chao 2015 kuelekea uchaguzi mkuu.
Dr Shein alisema “Napenda nipongeze juhudi zinazochukuliwa na chama chetu kwa viongozi wa chama chetu kukiimarisha chama hichi na kua imara zaidi kuliko changuzi za miaka iliyopita mara hii kukuwa kwa kasi zaidi na kuwa na matarajio makubwa ya ushindi mkubwa wa chama chetu. Ambapo Dr Shein alisema matarajio ya chama Cha Mapinduzi kushinda katika uchaguzi ujao ni kuanzia 52% hadi 58% kwa Zanzibar hivyo ni faraja kubwa. Baada ya kusema hayo alisema kikao kimefunguliwa na mkutano uko wazi wajumbe kuchangia’’.
Akaanza kusimama Dr Hussuen Mwenyi Waziri wa Afya na kumtaka Mh Rais pia afafanue mpasuko uliopo ambao unaonekana wazi kukiathiri chama cha Mapinzudi Zanzibar kuhusu Katiba mpya na kuhusu viongozi wa Jumuia ya Uamsho ambao wamefunguliwa mashtaka Tanzania Baraza jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limeonekana kukiathiri chama chao kwa watu walio wengi kuchukizwa na jambo hilo kwa upande wa Zanzibar.
Baada ya hapo alisimama ndugu Shaka Mwenyekiti vijana wa CCM na neno la kwanza alisema ‘’Mhe Rais chama chetu kimekufa. Akaendelea kusema ‘’Chama chetu kimekufa na aliyekiuwa chama hichi wewe.
Ndio aliposimama Mh Rais Dr Shein na kumwambia Shaka mbona wewe huna heshima maneno gani hayo unayosema kuniambia mimi. Unapaswa kuniheshimu na viongozi na marais wote wa Zanzibar mumekuwa mukiwa na heshima lakini mimi munakuwa munanivunjia heshima. Na ndio nyinyi mnaosema mimi sigombanii tena Urais wa Zanzibar na hali mimi mwenyewe sijatamka jambo hilo. Viongozi wote waliopita wa Zanzibar haijawahi kutokezea mtu CCM kusema kiongozi huyo hagombanii tena baada kumaliza kipindi cha miaka 5 isipokuwa mimi tu.
Naomba mara moja utoke nje na nitakuchukulia hatua kwa kunivunjia heshima na nitakuweka ndani ndipo Shaka alipotolewa nje chini ya ulinzi.
Ndipo sasa Aliposimama Asha Bakari mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akaanza kumpongeza rasi kwa juhudi za chama zilipofikia na kupiga hatua zaidi katika kuleta Maendeleo, na pia kumtaka Rais aweze kumsamehe Shaka amchukulie kama mtoto amekosea na mtoto akikosea kiganja hakikatwi bali huoshwa na akachukua ahadi watamwita ndugu Shaka ili kumuonya mara ya pili asirudie tena.
Kwenu wadau.
Jf
SOURCE;MZALENDONET
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment