Alan
Pardew ametajwa kuwa meneja bora wa mwezi wa 11 wa ligi kuu ya nchini
Uingereza mara baada ya kuiongoza vyema klabu yake ya Newcastle kupata
ushindi wa michezo mitatu kati ya minne aliyocheza ndani ya mwezi huo.
Pardew
ameiongoza timu yake kupata ushindi wa 1:0 dhidi ya Liverpool kwenye
dimba la St James' Park, kuwachapa klabu ngumu ya West Bromwich Albion
kwa jumla ya magoli 2-0 kwenye dimba lao la nyumbani la the Hawthorns
kabla ya kurejea nyumbani na kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Queens
Park Rangers nyumbani kwao St James Park.
Kilicho
nisukuma mimi kuandika makala hii ni hali ya mambo ilivyokua ndani ya
klabu ya Newcastle miezi kadaa iliyopita pale ambapo mashabiki wa timu
hiyo walikua wakiingia uwanjani wakiwa na mabango yanayowataka mabosi wa
klabu hiyo kumfungashia virago meneja huyo nhio sababu iliyonifanya
kichwa changu cha habari niseme "MPIRA HAUNA ADABU HATA KIDUCHU"
0 comments :
Post a Comment