Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe
amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaounda kamati hiyo,
kufanya kazi kama ilivyo kamati yake kwa Tanzania Bara.
Zitto aliyasema hayo kwenye semina ya
wawakilishi hao iliyofanyika jijini ambapo alisema, kamati
husimamia matumizi yote ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyoidhinishwa na baraza na kutoa taarifa zake kwa Umma.
Alisema hesabu za Serikali huendana na Ripoti ya CAG ambayo ndiyo nyenzo kuu ya Baraza katika kusimamia fedha za umma.
Hata hivyo, Zitto alisema PAC inapoona inafaa,
huagiza ukaguzi maalumu kwenye maeneo mahususi na njia hiyo imesaidia
kuibuliwa kwa mambo mengi ya ufisadi wa fedha za umma kwa Tanzania Bara.
“Kuna nyakati mkaguzi anakuwa haoni masuala fulani
hadi anapoombwa na vyombo vingine na hata wananchi…Ni vyema Kamati ya
PAC Zanzibar kutumia pia njia hii ili kuimarisha usimamizi bora wa fedha
za umma kwa Zanzibar kama ilivyo sasa katika Jamhuri ya Muungano,”
alisema Zitto na kuongeza;
“Ni muhimu kuzingatia kwamba wawakilishi ndiyo
chombo cha mwisho katika uamuzi kuhusu masuala ya wananchi wa Zanzibar
ikiwamo matumizi ya fedha za umma.”
Ni muhimu kuhakikisha kuwa Wizara ya Fedha ya
Zanzibar inajibu hoja za PAC (treasury notes) na hapo ndipo mzunguko wa
uwajibikaji unakuwa umekamilika.
Alisema ni wakati wa kufikiria namna ambavyo CAG
na PAC wanaweza kutimiza wajibu wao katika kuzuia matumizi yanayoelekea
kutokuwa na ufanisi.
0 comments :
Post a Comment