Eliakim Maswi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda , Eliakim Maswi, Katibu Mkuu
ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi
yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Sefue
amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia , Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa
kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma
wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa
amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya
Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)”ambapo
“Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma
wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Badala yake,
Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara
ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi
utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia
imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana,
Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma,
anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo
nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana
makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili
walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti
ya Tegeta Escrow.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa
pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO)
waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la
uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana
kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment