Mwenyikiti
wa wahisani ambaye ni balozi wa Finland nchini Tanzania ,Sinikka
Antila.Mjadala mkali umeingia siku ya pili nchini Tanzania kufuatia Rais
wa nchi hiyo Jakaya Kikwete kulihutubia taifa la nchi hiyo ambaye
pamoja na mambo mengine alitangaza kumfuta kazi waziri mmoja kwa
kuhusika na kashfa ya uchotaji wa mamilioni ya fedha kwenye account ya
Escrow.
Upande wa
upinzani umekosoa hotuba hiyo na kusema alipaswa kutangaza kuwafuta
kazi mawaziri na watendaji wengine waliotajwa kwenye azimio la bunge
lilipelekwa kwake hivi karibuni.Wakati haya yakiendelea wahisani
waliositisha misaada kufuatia kashfa hiyo leo wamesema wamepokea kwa
furaha hotuba hiyo na wametangaza kuanza kuipata Tanzania fedha asilimia
15 ya walizoahidi kwenye bajeti.
Rais wa
Tanzania Jakaya Kikwete alitangaza kumfuta kazi waziri wa Ardhi Prof
Anne Tibaijuka katika hotuba yake hapo jana ambaye ni mmoja ya mawaziri
wanaodaiwa kuhusika na kashfa ya ufisadi ya kuhamisha isivyo halali
fedha kwenya akaunti ya Tegeta Escrow.Hotuba hiyo Rais Kikwete tangu
jana imezua mjadala mkali nchini Tanzania ambao wengi wamekuwa na maoni
tofauti.
Chama
Kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimekosoa
hotuba hiyo na kusema kimesikitishwa na hatua alizozitangaza Rais
Kikwete hapo jana.Hivi karibuni Bunge la Tanzania liliapitisha maazimio
nane ambapo miongoni mwa maazimio hayo ilikuwa ni pamoja na serikali
kuwachukulia hatua ZA kinidhamu pamoja na kuwafuta kazi mawaziri na
maafisa wa serikali waliohusika katika sakata hilo.
Miongoni
wa watendaji hao ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo
Katibu Mkuu wa Wizara Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Profesa Anne
Tibaijuka ,Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania Tanesco pamoja na maafisa
wa na watendaji wengine waliohusika kwa namna moja au nyingine katika
sakata hilo.
Hata
hivyo katika hotuba hiyo Rais Kikwete mbali kumfuta kazi waziri huyo
mmoja wa Ardhi hakusema kama hao waziri mwingine aliyebaki ambaye ni
Waziri wa Nishati na Madini na Katibu Mkuu wake watachukuliwa hatua za
kinidhamu lini zaidi ya kusema anamweka kiporo waziri huyo huku
akisubiri uchunguzi dhidi ya waziri huyo jambo linalopingwa na upande wa
upinzani.
Wakati
hayo yakiendelea nchi wahisani wa nchi zipatazo 12 ambazo zilisitisha
misaada ya takribani dola milioni 500 kwenye bajeti ya Tanzania zimesema
kupitia kwa Mwenyikiti wao ambaye balozi wa Finland nchini Tanzania
Sinikka Antila zimesema kwa njia ya barua pepe kwa BBC kuwa nchi hizo
zimefurahishwa na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyokubali
kutekeleza maazimio ya Bunge na kusema kuwa kuanzia kuanzia leo
wamekubali dola bilioni 84 sawa na asilimia 15 ya mchango wao kwenye
bajeti ya Tanzania.
Kwa
upande mwingine upande wa chama kinachotawala CCM kupitia kwa Katibu
Mwenezi wa vijana wa chama hicho Paul Makonda amesema wanaipongeza
hotuba ya Rais Kikwete na hatua alizochukua.
Hotuba
hiyo ya Rais Kikwete huenda itaendelea kuleta mjadala Tanzania kwa siku
kadhaa kufuatia uzito wa kashfa hiyo ambayo imeitikisa taifa hilo.CHANZO:BBC
0 comments :
Post a Comment