-->

MICHEZO YA OLYMPIC KUANDALIWA KATIKA NCHI MBILI TOFAUTI

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC imepiga kura ya kuruhusu michezo ya Olimpiki kuandaliwa na nchi mbili na kuongeza michezo mipya kama sehemu ya mabadiliko mapana yanayofanywa na Rais Thomas Bach
IOC Treffen in Monaco 08.12.2014 Thomas Bach
Hatua hizo ni sehemu ya kampeni ya Rais wa IOC Thomas Bach yenye lengo la kuifanya michezo ya Olimpiki ya msimu wa Joto na Baridi kuwa rahisi kundaa na yenye kuvutia zaidi kwa umma wakati yakipambana na ongezeko la ushindani kutoka kwa watazamaji.
Bach amependekeza mageuzi 40, yanayofahamika kama Agenda 2020, ambayo yanapigiwa kura leo na kesho katika kikao maalum cha mashirikisho 104 wanachama wa IOC mjini Monaco.
Katika mabadiliko mengine, idadi ya wachezaji watakaoshiriki katika michezo ya Olimpiki ya msimu wa Joto ni 10,500, wakati nao wa Olimpiki ya msimu wa Baridi ikiwa 2,900, maana kuwa kama michezo mipya itaongeza, michezo mingine italazimika kupunguza idadi ya nafasi za medali.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
SOURCE:DW SWAHILI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment