Watu wengi hatujitambui tunaishi bila kujua maisha yetu binafsi yanakwenda wapi. Kutojitambua huko ndio chanzo cha wewe kubaki kila siku unahudumiwa na mama au baba kila kitu ukihisi bado mtoto mdogo, ukilalamika pesa huku wewe ni muhitimu wa chuo, umelemewa na madeni huku una elimu,huna uhuru wa kula na kununua kitu kisa huna pesa. Ndugu yangu jitambue uko wapi na unaelekea wapi weka ndoto na malengo,weka jitihada,tenga muda,mkabidhi mungu,epuka watu wenye mtazamo hasi,jiamini unaweza tenda miujiza, amini mabadiliko ktk maisha yanawezekana bila mtaji mkubwa,acha kubagua kazi kisa una elimu kubwa.
unapokuja kwenye suala la pesa ndg yangu elimu haina msaada sana kwani elimu ya pesa haifundishwi darasani na mitaala yetu inatuandaa na kutujengea fursa ya kutafuta ajira na wala sio kujiajili.
Sasa leo jitambue rafiki na ubadilike:
unapokuja kwenye suala la pesa ndg yangu elimu haina msaada sana kwani elimu ya pesa haifundishwi darasani na mitaala yetu inatuandaa na kutujengea fursa ya kutafuta ajira na wala sio kujiajili.
Sasa leo jitambue rafiki na ubadilike:
1. WATU WENYE MUDA MWINGI PESA HAWANA.
~Kundi hili linakera sana kwani ndio kundi pekee lenye mtazamo hasi katika jamii. Hawa watu wamekata tamaa na Kuridhika na maisha yao hawatambui umri unakwenda. Hawa ndio waangalia SERIES KILA KUKICHA,ndg yangu hizo ni designs za wenzako umeangalia miaka yote je mbona hujatengeneza series yako? Mara zote jifunze kutazama kitu kinacho kutimizia ndoto. Km wewe ni fundi nyumba angalia movies zinazo onesha jinsi gani majengo yakifahari yanavyokuwa designed, km wewe ni dr angalia vitu vinavyo ongeza ubunifu. Ndugu yangu waswahili wakisema TIME IS MONEY. Hahaha sasa chezea muda. Time ndio mtaji mkubwa wa masikini lkn masikini hajui hilo ndio mana hawalipwi kulingana na muda ila hulipwa kulingana na THAMANI YAKO.
Watu hawa ni wanafunzi, wahitimu,wacheza kamali, walevi wa mpira,vinywaji nk badilika rafiki muda wako ndio mtaji lkn hujatambua hilo.
2. WATU WENYE PESA NYINGI MUDA HAWANA
Kundi hili linakaliwa na watu wenye wazifa mkubwa hapa duniani. Km mabosi wa taasisi mbali mbali. Hivyo wanalipwa pesa nyingi lakini muda wote wamebanana na kaxi. Sasa nauliza ~hizo pesa unatafutia wajukuu? Km jibu ni hapana acha kuwaza kuwa katika kundi hili~ asilimia 99.99 ya wasomi wana fikra potofu ya kuja kuchukua madaraka makubwa hapa duniani. Hawajui kuwa pesa anayo itafuta haifurahii hata siku moja, Anakuja usiku nyumbani pia anaondoka usiku, hata kufurahia maisha ya pesa na mama watoto hakuna, Mbona uteswe na pesa na kuwa mtumwana pesa ambazo huxifaidi?
3. WATU AMBAO HAWANA MUDA NA PESA PIA HAWANA.
Hahahaha hili ni kundi ukiwaomba pesa anakwambia~SUBIRIA MWISHO WA MWEZI~ Napenda kurudia tena elimu ya pesa haifundishwi darasani bali mtaani. Ndio mana wakoloni walituletea elimu na ajira. Wengi waliopewa ajira walikua na majivuno na kuwalingia watu ndio hadi leo hii ajira za kikoloni zinawateka mpaka wasomi wakubwa. Amini usiamini ujuzi mmoja hawakupeleki kwenye mafanikio. Ndugu,mwalimu,hakimu,daktari,engineer,afisa,mhasibu mbona unateseka muda mwingi kazini unalipwa pesa ndg kiasi hicho?hivi umefikia kuwa mnyengo kiasi hicho?? MUDA MWINGI KAXINI PESA KIDUCHU
Ndugu yangu jiulize tangu uanze kazi umejikwamua wapi kama sio kuuingia katika madeni wasiyo na msingi? Mbona uendelee kuteseka bila mafanikio? Wafanyakazi hawa hutafuta pesa ya kujikimu sio ya maisha yake yote.
4. WATU WENYE PESA NA WANA MUDA
Hahahaha napenda sana hili kundi na najisikia nina nguvu ya maajabu kwani nina amini niko katika kundi hili. Kundi hili ni watu wanao furahia PESA WANAYO ITAFUTA. Hawa ndio asilimia 5 tu ya watu duniani. Hawa ni watu waliojiajili na wana miradi mikubwa. Pesa inawatumikia ndio mana wana uhuru wa kukaa na familia,kutoka out na nje ya nchi. Rafiki yangu mbona usifurahie pesa yako? Ndugu yangu maisha ni magumu hutaki kuhamia kundi hili
0 comments :
Post a Comment