-->

MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE ASALIM AMRI,NI BAADA YA KUHUSISHWA NA ESCROW

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, amesalimu amri ambapo ametoa msimamo wake kuwa, yupo tayari kuachia nafasi ya uenyekiti kwani ni maamuzi ya Bunge.
Kauli ya Mwambalaswa inakuja siku moja tu, baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuweka wazi wenyeviti watatu wa kamati za Bunge ambao wanatuhumiwa kwenye sakata la Escrow wanatakiwa kuachia ngazi nafasi hizo.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu, Mwambalaswa alisema tayari Bunge limetoa maazimio, hivyo ni lazima ayaheshimu na kuyatekeleza maana ni sehemu ya Bunge ambalo limetoa mapendekezo hayo.
Mwambalaswa ambaye ni Mbunge wa Lupa mkoani Mbeya, alisisitiza hawezi kupingana nayo, bali kinachohitajika ni kupisha wengine ili kazi za kamati ziendelee.
Alisema yeye ni mtu anayetambua maana ya uwajibikaji, hivyo ili kuhakikisha maazimio hayo yanaheshimiwa ni lazima akubaliane nayo kwa maslahi ya Bunge na taifa.
“Wakati maazimio ya Bunge yakitolewa, nilikuwa miongoni mwa wabunge tuliotoa mapendekezo hayo, hivyo siwezi kuyapinga na nipo tayari kwa uamuzi huo na ndiyo maana ya uwajibikaji,” alisema.

Ndugai wakati akiwazungumzia wenyeviti hao, juzi aliliambia gazeti hili kuwa, watu wote ambao wapo kwenye mamlaka ya Bunge na wanahusishwa na Escrow, lazima waachie nafasi ya uenyekiti wiki mbili, kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge.

Vikao vya Bunge vinatarajiwa kuanza Januari 27, mwakani mkoani Dodoma na kabla ya hapo, kutakuwa na vikao vya kamati ambavyo vitafanyika Dar es Salaam.



Chanzo:jamboleo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment