-->

DONDOO ZA AFYA:HII NDIO TIBA PEKEE YA MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI

    Maumivu ya tumbo chini ya kitovu husumbua wasichana na wanawake wengi wakati wa hedhi zao. Maumivu haya yanaweza kuwa kidogo au wakati mwingine kuwa makali sana kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya shughuli nyingine.
Maumivu ya Tumbo Yanavyotokea
Maumivu haya hutoka kwenye tumbo la uzazi. Wakati wa hedhi ukuta wa mji wa mimba huanza kubomoka na kisha kusababisha damu kutoka. Wakati ukibomoka misuli ya tumbo la uzazi hukaza na kusinyaa, kukaza huku ndiko kunakosababisha maumivu wakati wa hedhi.
Licha ya maumivu haya kusababishwa  na kukaza kwa tumbo la uzazi, kuna magonjwa mengine yanaweza kuchangia kuleta hali hii. Mara nyingi maumivu ya namna hii huwa makali zaidi kiasi cha kumfanya mtu ashindwe kuendelea na shughuli zake. Hali kama;
  • Endometriosis (uwepo wa tishu za ukuta wa mji wa mimba sehemu nyingine kama kwenye ovari au misuli ya mji wa mimba)
  • PID (Maambukizi kwenye via vya ndani vya uzazi)
huweza kuchangia kuleta hali hii.
Matibabu
Matibabau ya hali hii inategemea na kiasi cha maumivu. Kama maumivu ni kidogo, yanaweza kuvumiliwa na baada ya hedhi kuisha. Njia nyingine za kupunguza maumivu wakati wa hedhi;
  • Kukanda tumbo kwa maji ya moto
  • Kunywa kinywaji chenye moto
  • Usinywe vinywaji vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa
  • Tumia dawa za kuzuia maumivu kama Paracetamol au Buscopan.
Unapoona unapata maumivu makali sana ni vizuri uonane na mtaalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Au wasiliana nasi kupitia namba +255 785 494 456
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment