Maelfu ya watu wanatarajiwa
kuandamana katika bara-bara za miji ya Washington na New York kupinga
mauaji ya wanaume weusi wasiokuwa na silaha yaliyofanywa na polisi wa
Marekani, ili kulitaka bunge lilinde wananchi.
Taarifa iliyotolewa
na kiongozi wa kutetea haki za raia, Al Sharpton, ilieleza kuwa bunge
linahitaji kuchukua hatua kubadilisha sheria na hali bara-barani.Kati ya wataohudhuria maandamano hayo ni familia za Michael Brown, kijana aliyeuwawa katika jimbo la Missouri, na Eric Garner, ambaye alikufa wakati anakamatwa mjini New York.
Kesi za askari polisi waliohusika na vifo hivyo zilifutwa na kuzusha maandamano kote Marekani.
0 comments :
Post a Comment