Ni dhahiri kuwa watu wengi tumekata tama na afya zetu na tumezoea kukaa na matatizo ya kiafya bila kujali afya yako unaipeleka wapi. Moja ya kitu ambacho unatakiwa kufahamu ni kuwa dalili ndogondogo ni ishara ya ugonjwa sugu utakao kupata mbeleni.watu wengi hatuwezi kubaini ni jinsi gani miili yetu imedhoofika kwa kushambuliwa na magonjwa hadi pale afya yako itakapo boreka.
Zifuatazo ni miongoni mwa dalili ambazo ni viashiria kuwa kuna tatizo la kiafya linaendelea mwilini hivyo kitendo cha kutibu dalili tu ni dhahiri kuwa unafanya ugonjwa huu ukomae na hatimaye tiba yake iwe changamoto. Unapotaka kuboresha mwili wako unatakiwa kujua kuwa mwili wako umeundwa na ogani mbalimbali ambazo hufanya kazi kwa pamoja kama mfumo mmoja. Hivyo endapo kiungo kimoja kikipata hitirafu ni dhahiri kuwa kinaweza athiri utendaji kazi wa ogani zingine za mwili. Hivyo basi kitendo cha kutibu dalili ndogo ndogo kwa kutumia dawa mbalimbali ni dhahiri kuwa unazidi kuhatarisha afya yako
Inaweza kuwa unasoma makala hii na unahisi kukata tama na afya yako kwa kusumbuka na dalili ndogondogo ambapo kila ukipima vipimo vinaonesha huna ugonjwa. Lakini leo ningependa nikwambie kitu kuhusu namna y a kuboresha afya yako na kurudi katika afaya yako kama ulivyo kuwa mwanzo.
Kumbuka kuwa dalili ndogo ndogo ni ishara kuwa mwili unashambuliwa na magonjwa sugu hivyo hatua maalumu zinatakiwa zichukuliwe kuunusuru mwili wako. Ni dhahiri kuwa miili yetu tunaishi katika mazingira yenye sumu mbalimbali, tunakula vyakula vilivyo nyunyuziwa dawa mbalimbali wakati wa ulimaji wake hadi kuvunwa kwake,pia tunaishi katika mazingira yaliyo jaa sumu mbalimbali,tunaishi kwa kunywa dawa zenye sumu mwilini mwetu. Wengi huupa mwili kazi zote hizi kwa sababu ini kazi yake kubwa ni kuundoa sumu mwilini. Lakini inatakiwa utambue kuwa ini linapozoofika linazidiwa na kitendo cha kuondoa sumu mwilini na hivyo mwili unahitaji msaada wako ili uweze kufanya kazi ipasavyo. Ni changamoto pia kwa watu wengi wanopenda kupunguza uzito bila kujua kuwa miili yao imejaa sumu mbalimbali yani FREE RADICALS ambazo zimekuwa ziki athiri utumikaji wa chakula mwilini na hatimaye kusababisha mrundikano wa mafuta yasiyo faaa mwilini mwao. Watu wengi siku hizi wamekuwa wakitaka kutumia virutubisho mbali mbali ili tu kwamba wapungue uzito. Changamoto kubwa ni kwamba kama tayari umeshaanza kuonyesha dalili za mwanzo za kisukari aina ya pili yani PRE DIABETES ni dhahiri kuwa utapungua kilo chache ukilinganisha na Yule ambaye hana dalili za kizuizi cha insulin yani INSULIN RESISTANCE. Hivyo kama tayari umesha wahi tumia hivyo virutubisho na hukupungua sana ningependa uchukue hatua kuhusu afya yako kwani wengi hukaa na kuanza kulaumu kuwa hivyo virutubisho havifanyi kazi.
Pia dalili zifuatazo zimekuwa si tishio kabisa kwa binadamu kwani wengio wanaamini kuwa ni udhuru mdogo tu mwilini bila kujua kuwa miili yao inashaambuliwa na magonjwa sugu bila wao kuchukua hatua. Kwani takwimu zinaonesha kuwa dawa pekee zinazo ongoza kununuliwa madukani ni dawa za kupunguza maumivu . Mmoja wa mkufunzi wangu mzungu kutoka Amerika alikuwa anatuzuia kutoa dawa ya paracentamol kwa watoto wote walioletwa kupata matibabu hospitalini. Sikujua nini sababu lakini nilipokuja kumuuliza akasema unapompatia mototo dawa hii homa itashuka na maumivu kupungua lakini sio kweli mototo amepata nafuu bali umefunika ugonjwa wake na kudanganya kuwa nafuu imepatikana. Lakini sisi dawa kama hizi imekuwa ni chakula cha kila siku ili uweze kufanya kazi za kila siku.
Basi leo ningependa kukutajia dalili ambazo ni ishara kuwa mwili wako unasumbuliwa na ugonjwa mkubwa na hivyo suluhisho mahususi linahitajika kuondoa tatizo
1. Uchovu wa bila sababu
2. Matatizo ya mfumo wa chakula kama choo kigumu,tumbo kujaa gesi,kiungulia
3. Maumivu ya kichwa na mifupa
4. Allergy
Hizi ni dalili zinazoashiria kuwa mwili wako umelemewa na ugonjwa na imekuwa changamoto kuwa watu wengi wenye matatizo kama haya mara nyingi huambiwa hawana ugonjwa wowote na hivyo hukata tamaa.
ZIFUATAZO NI HATUA NNE AMBAZO UNATAKIWA KUZINGATIA ILI KUBORESHA AFYA YAKO
1. Tambua jinsi gani chembe chembe za mwili za urithi zinavyo weza kuboreshwa na kuharibiwa na vyakula tunavyokula na mazingira tunayoishi. Kwani watu wengi tumekuwa tukipenda kutumia vyakula vinavyo athiri mwili na kuwa tayari kutumia pesa yako kutibu ugonjwa badala ya kuboresha afya yako na kuepuka na magaonjwa.
Vifuatavyo ni vitu ambavyo vinaweza athiri mwili wako na hatimaye kusababisha magonjwa sugu.
a) Lishe
b) Hewa,maji,mazoezi
c) Ajali
d) Matatizo ya kisaikolojia
e) Sumu kutoka kwenye mazingira
f) Wadudu wa maambukizi
g) Mionzi ya simu,tv na vitu vingine vya electronics
Vitu hivi huathiri na kupeleka taarifa kwa chembeche za urithi yani GENES na hatimaye kubadili utendaji kazi sahihi wa hizi genes na hatimaye kusababisha magonjwa mbali mbali. Ni dhahiri kuwa watu tunarithi chechembe hizi kutoka kwa wazazi wetu hivyo ni jukumu letu kuhakikisha hizi genes hatuzichokozi kuweza kusababisha magonjwa sugu. Na kitu kikubwa ambacho huchokoza genes hizi za kusababisha magonjwa sugu ni vyakula tunavyokula. Hivyo chakula unachokula kinaweza kuwa ni tiba au ni sumu ndogo ndogo inayo enda kusababisha magonjwa sugu mwilini. Vyakula kama vyenye sukari ngingi, vinywaji vya sukari nyingi, vyakula vya mikate mweupe, vyakula vya vyama kwani vimekuwa ni visababishi vikubwa vya watu kuugua magonjwa kama, mizunguko ya hedhi mibovu,kichwa kuuma ovyo, macho,uzito kupita kiasi,kisukari,shinikizo la damu,kukosa nguvu za kiume nk. Yote haya ni kutokana na kula vyakula vinavyo athiri utendaji kazi wa genes za miili yetu.
2. Unatakiwa kutambua namna vichocheo au hormone za mwili wako zinavyo athiri utendaji kazi wa mwili wako na kusababisha magonjwa pia ni muhimu kujua namna gani utendaji kazi wa ubongo wako utakavyo weza kuathiriwa na hatimaye kusababisha magonjwa sugu katika miili yetu. Ni ukweli usiopingika magonjwa mengi sasa hasa ya mizunguko mibovu ya hedhi,kansa,uvimbe kwenye kizazi ,ukosefu wa nguvu za kiume na kike,kutopata mototo husababishwa na vichocheo vya mwili kuvurugika na hatimaye kusababisha magonjwa haya yote ambayo sasa ni changamoto kwa tiba zake mahospitalini. Utafiti uliofanyika hivi punde unaonesha kuwa matumizi ya vyakula vya sukari nyingi vinamfanya mtu kuwa addicted yani kudhurika na hatimaye kutumia vyakula hivi kupita kiasi. Kwa ufupi sukari inapokuwa nyingi kwenye damu husababisha uchovyaji wa kichocheo cha insulin ambacho huja kuhifadhi mafuta katika tumbo yani BELLY FAT na sehemu zingine za kuhifadhia mafuta na hatimaye kusababaisha uchovyaji wa kichocheo cha CORTISOL ambacho huja kuzuia utolewaji wa kichocheo cha LEPTIN ambacho hutolewa na seli zinazohifadhi mafuta na kazi yake kuu ni kusaidia kusawazisha hamu ya chakula kwa kupeleka taarifa kwenye ubongo kuwaonesha kutosherezwa na chakula. Hii inaweza ikawa ni sababu kubwa inayokupelekea kula mara kwa mara kunako sababishwa na njaa za mara kwa mara kutokana na LEPTIN hormone kuwa chini. Pia sukari nyingi kwenye damu husababisha utoaji wa insulin nyingi ambayo hupunguza vichocheo vya TESTOSTERONE ambavyo ni vichocheo muhimu katika mwili wa mwanaume. Kwani kichocheo hiki ndicho kinachokusaidia uwe na sifa zote za jinsia ya kiume pia inakusaidia kuwa na matamanio kutoka jinsia tofauti,nguvu wakati wa tendo la ndoa na kutengeneza mbegu za kiume. Hivyo ni dhahiri kuwa ongezeko la vyakula vingi vya sukari viwanadani ndio visababishi vikubwa vya KUPUNGUA KWA NGUVU ZA KIUME KWA VIJANA WENGI. Pia kuvurugika kwa vichocheo vya kike kunasababishwa na hivi vyakula vya sukari nyingi vyakula vya viwandani na vinywaji vyenye vionjo lukuki ni hatari na ndivyo chanzo cha magonjwa mengi kwa wanawake yanayo ambatana na kuvurugika kwa vichocheo vya kike. HIVYO ILI KUBORESHA AFYA YAKO CHUKUA HATUA YA KUREKEBISHA MZUNGUKO WAKO NA MATATIZO MENGINE KWA KUWEKA SAWA VICHOCHEO VYAKO VYOTE VYA MWILI KATIKA HALI YA USAWA. Kwani aina ya uvimbe mbali mbali katika miili yetu mara nyingi husababishwa na mrundikano wa vichocheo vya miili yetu na hatimaye kusabisha magonjwa. Miongoni mwa uvimbe unao sababishwa na vichocheo kuvurugika hasa vya estrogen ni UVIMBE KWENYE KIZAZI,KANSA YA SHINGO YA KIZAZI, KANSA YA TUMBO LA KIZAZI NA KANSA YA TITI hivyo rekebisha vichocheo vyako uepuke magonjwa sugu kama haya kwani kitendo cha kuutoa uvimbe sio suluhisho kwani mvurugiko wa vichocheo upo palepale na hivyo uwezekano wa uvimbe kurudi tena upo kwa asilimia kubwa na ningependa kukwambia kuwa suluhisho ni kupambana na mvurugiko wa vichocheo hivyo na kuchukia uvimbe huku ukiacha chanzo cha tatizo na kukimbilia kutoa matokeo ya tatizo.
3. Tambua kuwa mfumo wa mmeng”enyo wa chakula ndio kiini cha afya yetu. Watu wengi tunashindwa kutambua kuwa huu ndio mfumo pekee unao kutana na maradhi mbali mbali kabla hata hayo maradhi hayajafika mbali katikamiili yetu. Hivyo ni mfumo ambao umehatarishwa kulingana na mahali ulipo hivyo unakabiriliwa na changamoto nyingi kutokana na vyakula tunavyokula ambavyo vimejaza sumu mbali mbali yani HEAVY METAL ambazo hizi zikiingia mwilini zinaathiri utendaji kazi wa mwili na hatimaye mwili kuanza kuonesha dalili ndogo ndogo ambazo vipimo vyake huonesha huna madhara yoyote. Hivyo ni kujumu lako kulinda mfumo huu kwani ni mfumo pekee ambayo ndio kiini cha afya yako. Kuna vyakula vinatakiwa kuepukwa kabisa kwa mafano vyakula vitokanavyo na ngano nyeupe vina kiini kiitwacho GLUTEN ambayo ni protini ngumu kumeng”enywa na enzyme au vimengenya chakula vya mwili. Na hivyo mfumo wa chakula huanza kupambana na kiini hicho na hatimaye kusababisha kuvimba kwa kuta za utumbo au mfumo wa chakula na hatimaye kufanya protini hiyo kupenya na kusababisha mwili mzima kutengeneza mpambano wa hicho kiini cha gluteni yani SYSTEMIC INFLAMATION. Kitendo hiki kinavuruga karibia shughuli zote za mwili hasa za utumiaji chakula yani metabolism na ndio chanzo kikubwa cha magonjwa sugu hapa duniani kama uzito kupita kiasi,mizunguko mibovu,kisukari aina ya pili, shinikizo la damu,mwili kuuma ovyo,kichwa kuuma,macho kuuma na kutokuona vizuri. Hivyo vyakula kama hivi vinavyo sababisha mpambano wa namna hii ni hatari kwa afya yako. Pia kuna vyakula vyenye metal au elementi nzito ambazo ni sumu katika miili yetu kwa mfano MERCURY, ARSENIC hivyo ni jukumu letu kuondoa hizi elementi kwani ndio chanzo cha magonjwa kama , mwili kuuma ovyo,kichwa ,uchovu bila sababu maalumu,kukosa nguvu za kiume,mzunguko mbovu,kinga ya mwili kushuka,kansa mbali mbali na uvimbe mbali mbali bila kusahau ugonjwa wakusahau ovyo. Haya yote unaweza kuyashinda kwa kupata elimu nzuri ya lishe ya namana ya kutumia nafaka ambayo haijakobolewa,kuepuka vyakula vya sukari nyingi pia vinywaji,kuepuka vyakula vya viwandani kula vyakula vingi vitokanavyo na MIMEA NA MATUNDA nina imani elimu bora ya afya yako itakuweka mbali na daktari na utapunguza matumizi ya pesa kutibu magonjwa kwa kunufaisha mifuko ya watu waliojitengenezea kliniki ambazo zote zinalenga kutibu mtu bila kumpatia elimu ya lishe bora.
4. Tambua kuwa tiba za dawa zakisasa ni nzuri endapo tu uko katika hali mahututi yani umezidiwa,umevunjika mguu, una maambukizi makali ni dhahiri kuwa chaguo lako la tiba lazima liwe tiba ya kisasa ya kutumia dawa hizi zenye chemikali. Lakini dawa hizi zimeonesha kuwa na changamoto hasa pale tunapotaka kutibu magonjwa sugu kwani nyingi zinalenga kutibu dalili na kuacha chanzo cha ugonjwa ukiwa unazidi kuwa sugu. Elimu bora ya namna ya kujinga na magonjwa ni muhimu sana kwani unapowekeza katika afaya yako hiyo ndio siri kubwa ya nchi zilizo endelea zilivyo ongeza umri wa kuishi. Elimu ya afya ni silaha ya kukuepusha kukutana na adui dakatri na kupunguza msongamano wa wagonjwa mawodini ambayo ni changamoto kubwa kwa madaktari wa hapa Tanzania. Hivyo ili tuweze kukidhi kiasi cha madaktari wa hapa Tanzania bila uhaba wowote ni kuwekeza katika elimu ya afya ya lishe yako sio kuwekeza fedha ya kwenda kupima mara kwa mara kwani kupima sio suluhisho la magonjwa bali KUILINDA AFYA YAKO KWA KUWA NA ELIMU YA LISHE BORA NA KUUPA MWILI WAKO VYAKULA SAHIHI.
ASANTE BY FRANK ALFRED KARIBUNI KATIKA JUKWAA LA AFYA ELIMU +255 785 494 456
0 comments :
Post a Comment