-->

MATUKIO KATIKA JINSI HALI ILIVYOKUWA DUMILA KWENYE MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Baadhi ya watuhumiwa wa vurugu za kufunga barabara kuu ya Morogoro- Dodoma
kwa mawe na kuchoma matairi eneo la Dumila, Tarafa ya Magole, wilayani
Kilosa, jana kulikofanywa na wakulima wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa kikosi cha
kutuliza ghasia (FFU) baada ya kukamatwa kwao.

Baadhi ya magari yakipita barabara kuu ya Morogoro- Dodoma eneo la Dumila,
Tarafa ya Magole, wilayani Kilosa jana baada ya Polisi kurejesha  hali ya
usalama  kwa kuondoa vizuizi vilivyowekwa na wakulima.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Morogoro akiwadhibiti
vijana walituhumiwa kufanya vurugu  za kufunga barabara kuu ya Morogoro-
Dodoma kwa mawe na kuchoma matairi juzi  katika eneo la Dumila, Tarafa ya
Magole, wilayani Kilosa, na kusababisha adha kubwa wa watumiaji wa barabara
hiyo kwa muda wa saa sita.
( Picha zote na John Nditi).

Mkuu wa  Kikosi cha Askari wakutuliza Ghasia (FFU) , mkoani Morogoro,
akiwatangazia wananchi kutawanyika mara moja
kutoka eneo hilo au la Polisi itatumia nguvu
kuwatawanya .
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment