Kocha wa
Real Madrid, Muitaliano Carlo Ancelotti ameelezea uwepo wa Cristiano
Ronaldo’s katika kikosi chake kama faida baada ya nyota huyo kufunga
goli tatu peke yake (Hat-trick) na kufikisha jumla ya goli 200 katika
kigi hiyo wakati madrid ilipoishindilia Celta Vigo 3-0.Katika pambano
hilo, nyota huyo toka ureno, Cristiano Ronaldo alifunga goli zote tatu
na hivyo kuvunja rekod ya hattrick ya la liga akifikisha 23, moja zaidi
ya Magwiji Alfred Di Stefano na Telmo Zarra, huku zikiwa tatu zaidi ya
mpinzani wake wa karibu Lionel Messi mwenye 20. Ikumbukwe nyota huyo
sasa amefikisha jumla ya goli 200 katika michezo 178 pekee ya La Liga
aliyoshiriki ikiwa ni kasi zaidi ya nyota yeyote.
Katika
mechi hiyo nyota huyo aliaanza kufunga kwa penati kufuatia kuvutwa eneo
la hatari kunako kipindi cha kwanza na hivyo kutokufanya ajizi kuujaza
mpira huo kimiani, kabla hajaongeza la pili na la 3 kipindi cha pili
akimalizia krosi ya nota kukota Brazil, Marcelo.
Mpaka
sasa nota huyo amefunga jumla ya magoli 23 katika michezo 24 ya la liga
msimu huu huku ushindi wa jana ukiiwzesha miamba hiyo (Real Madrid)
kuwafikia wapinzani wao Barcelona kwa kuishinda Celta vigo mara 18
mfululizo rekodi iliyowekwa chini ya mholanzi Frank Rijkaard msimu wa
2005-06. Klabu hiyo inaivaa timu toka ubeeligiji Ludogoretz jumanne na
kama itashinda itakuwa imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya
kihispania kushinda mfululizo katika michuano mbalimbali
0 comments :
Post a Comment