-->

MANCHESTER UNITED HII HAISHIKIKI,WAMTWANGA STOKE CITY 2-1

Ratiba ya ligi kuu ya England imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa usiku wa leo katika viwanja tofauti nchini Uingereza.
 Wakitoka kupata ushindi wao dhidi Hull City, Manchester United leo iliwakaribisha Stoke City kwenye uwanja wao Old Trafford katika mechi ambayo imeisha hivi punde.
Matokeo ya mechi hiyo ni ushindi wa 2-1 kwa vijana wa Louis Van Gaal – ukiwa ni ushindi wao wa nne mfululizo kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miezi 12. 

Magoli ya Maroune Fellaini na Juan Mata yalitosha kuendelea kuwamairisha Manchester United katika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 25. 

Nzozi aliifungia Stoke City goli la kufutia machozi kwenye mchezo huo.
BOFYA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE ZA MICHEZO
                                                 BUSATI LA MICHEZO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment