-->

MTOTO WA MIEZI NANE ALIYEIBIWA NA BIBI ASIYEFAHAMIKA APATIKANA KIBITI


 MTOTO JUMA OMAR JUMA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKA NYUMBANI KUTOKA KIBITI ALIPO IBWA.

Hatimaye mtoto Juma Omar Juma aliyeibwa amepatina jana.

Mtoto huyo mwenye umri wa miezi minane aliibwa ijuma iliyoyopita maeneo ya Mbagala Kizuwiani Jijini Dar es salaam.

Akisimulia mkasa huo mbele ya mwandishi wa munira blog Muhamed Khatib baba mdogo wa mtoto huyo alisema siku ya Ijumaa mama wa mtoto akiwa anafua nguo,alimuagiza binti yao (Lidya mwenye umri wa miaka kumi) akamchukulie maji bombani.

"Yule bint akambeba mtoto na kwenda naye bombani,njiani akakutana na bibi mmoja aliyedai kwamba mama yako nacheza naye mchezo kwa hiyo nina pesa yake nikupe umpelekee"Alisema.

Akiwa kashika elfu kumi akamwambia watafute chenji ambapo katika kutafuta huko wakafika hadi kiburugwa na hatimaye kufika mbagara rangi tatu.

"Njiani akamwambia yule bint nikusaidie kumbbeba mtoto na walipofika mbagara rangi tatu kituo cha mabasi ya kwenda shamba akampa (lidya) shilingi mia tano ili amnunulie juisi mtoto naye alifanya hivyo lakini alipo rudi hakumkuta yule bibi",alisema.

Aliendelea kusimulia kwamba mtoto Lidya alitaharuki sana kwani hakujuwa pale alipo hadi alipo pata msaada wa polisi jamii na kumpeleka kituo cha polisi mbagala kizuwiani na hatimaye kufika kwao.

Naye Omar Juma ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo alisema walipata taarifa kutoka polisi kwamba kuna mtoto ametelekezwa huko Kibiti,ndipo tukaenda na kumkuta akiwa amehifadhiwa katika kituo cha Polisi.

Alisema kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mwizi huyo alimtelekeza mtoto huyo baada ya kumuona analia mara kwa mara.ndipo wasamaria wema wakamuokota na kumpeleka polisi.

 Hivi sasa ndiyo tumerudi na tumemuacha Mwizi akiwa kituo cha Polisi Chang'ombe na kesho atafikishwa mahakamani,alisema bwanaOmar ambaye ni mwanafunzi mwandamizi wa madrasat Salama ya mbagala kizuwiani.

Aliongeza kusema"Tuna shukuru tumerudi na mtoto hali yake ni mzuri kimuonekano wa macho japo huyo mwizi kamnyoa nywele zote mtoto wetu",Alisema


Kabla ya kufika nyumbani kwa bwana Omar,munira blog ilianzia kituo cha polisi cha kizuwiani na kuambiwa "tumeomba mtuhumiwa afikishwe Chang'ombe polisi kwani bado tuna kumbukumbu ya watu kutaka kukichonma moto kituo chetu,alisema Polisi mmoja aliyekataa kutaja jina lake.



MTOTO LIDYA (DADA MLEZI)  NDIYE ALIYE HADAIWA NA HATIMAYE KUIBWA MTOTO






BWANA OMAR JUMA,BABA MZAZI WA MTOTO ALIYEIBIWA.


WANA NDUGU WAKIWA PAMOJA JANA USIKU MUDA MFUPI BAADA YA KUPATIKANA MTOTO OMAR

CHANZO:MUNIRA MADRASA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment